Home BUSINESS RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA BoT MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA ZANZIBAR

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA BoT MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Kisiwani Unguja kuanzia Januari 7-19, 2024.

Kupitia Maonesho hayo Benki Kuu inaelimisha wananchi kuhusu sera za uchumi na fedha; uwekezaji katika dhamana za serikali; usimamizi wa fedha binafsi, akiba, mkopo; namna BoT inawalinda watumiaji wa huduma za fedha; utunzaji sahihi wa noti na utambuzi wa alama za usalama; mifumo ya malipo ya taifa na namna Bodi ya Bima ya Amana inavyokinga amana za wateja wa benki na taasisi za fedha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here