Home SPORTS MOROCCO 3-0 TAIFA STARS, AFCON

MOROCCO 3-0 TAIFA STARS, AFCON

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza mchezo wa kwanza wa kundi F baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco katika mashindano ya kuwania taji la Mataifa ya Afrika 2023 uliochezwa leo Januari 17, 2024 nchini Ivory Coast.

Morocco imeanza safari ya kusaka kombe la Afrika dhidi ya Tanzania
wakiwa na wachezaji kumi na moja walioanza chini ya uongozi wa Regragui, waliojaa nyota katika kila nafasi – Hakimi katika safu ya ulinzi, safu ya kiungo iliyowashirikisha Amrabat na Ounahi, na wachezaji watatu wa kukera na Abde-En Nesyri-Ziyech, huku Tanzania ilijikuta ikifungwa 1-0 katika kipindi cha kwanza.

Baada ya mchezo wa Taifa Stars Miroshi kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 70 Morocco walipa ahueni kwani ndani ya dakika nne tu, walifunga mabao mawili, na hivyo kuhitimisha mechi hiyo kwa ushindi wa mabao 3-0.

Kufatia ushindi huo Morocco imeanza kampeni yao ya AFCON 2023 kwa kasi kubwa, ikibaki kuwa kinara katika Kundi F.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here