Home SPORTS DR-CONGO 1-1 ZAMBIA, AFCON

DR-CONGO 1-1 ZAMBIA, AFCON

Miamba miwili ya soka Afrika, Timu ya Taifa ya DR Congo na timu ya Taifa ya Zambia Chipolopolo, zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa mwisho wa kundi F ya mashindano ya AFCON nchini Ivory Coast.

Chipolopolo ndio ilikuwa timu ya kwanza kuzifumania nyavu za DR Congo dakika ya 23, goli likifungwa na kiungo fundi, Kings Kangwa.

Iliwachua dakika 4 DRC kusawazisha goli hilo kwa kufanya shambulio la kushtukiza ambapo mshambuliaji wa kulia wa timu hiyo Cedric Makambo, akipachika bao hilo kwakumalizia pasi kutoka kwa Garry Kakuta katika Dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo, na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko wakiwa na matokeo sawa.

Kipindi cha pili timu zote zilicheza kwa kushambuliana na kufanya mabadiliko kadhaa ya wachezaji ambapo DRC walimpumzisha Garry Kakuta na kumuingiza Meshack Elia, dakika ya 70, huku Zambia wakimpumzisha Lameck Banda akichukua nafasi ya Lumambo Musonda dakika ya 75.

Matokeo hayo yameifanya timu ya Morocco kuongoza kundi F ikiwa na alama 3, baada ya kuifunga Tanzania mabao 3 -0 katika mchezo wa awali, ikifuatiwa na Zambia na Congo zenye alama 1, huku Taifa Stars ikishika nafasi ya nne bila alama.

#Afcon2024
#afcon
#soccerafrica
#soccerzambia
#chipolopolo🇿🇲🇿🇲⚽️⚽️
#drcongo

Previous articleMOROCCO 3-0 TAIFA STARS, AFCON
Next articleSERA ZA UCHUMI ZA RAIS SAMIA ZALETA MATUNDA MAKUBWA NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here