Home SPORTS MLANDEGE BINGWA MAPINDUZI CUP KWA MARA YA PILI

MLANDEGE BINGWA MAPINDUZI CUP KWA MARA YA PILI

Klabu ya Mlandege ya Visiwani Zanizabar imefanikiwa kunyakua ubingwa wa kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo kwa kuichapa timu ya Wekundu wa Msimamizi Simba SC bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo.

Mchezo huo umepigwa katika Dimba la New Amani Complex Januari 13 Mjini Zanizabar majira ya saa 2.15 usiku.
Goli la Mlandege lilipachikwa kambani na mshambuliaji wake wa Kimataifa Joseph Akandwano katika kipindi cha pili cha mchezo huo akipangua safu ya ulinzi ya Simba.
Fainali hizo ni za 18 toka kuanzishwa kwa michuano hiyo ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matumufu ya Zanizabar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here