Home LOCAL MENEJA TARURA MKOA WA MOROGORO AAGIZWA KUANZA USANIFU WA BARABARA NA UJENZI...

MENEJA TARURA MKOA WA MOROGORO AAGIZWA KUANZA USANIFU WA BARABARA NA UJENZI WA MIFEREJI KILOSA

Kilosa.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Ndyamukama ameagizwa kuanza mara moja usanifu wa barabara ya Magole Estate-Mfuru pamoja na ujenzi wa mifereji ya maji katika mji wa Kilosa.

Agizo hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya barabara na mifereji ya maji iliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani hapa ambapo katika ukaguzi huo aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi.

Katika Kata ya Kitete walijionea uharibifu wa Barabara ya Magole Estate-Mfuru yenye urefu wa Km. 4.5 na Kata ya Mbuni walijionea mfereji wa maji unaosababisha mafuriko ya maji maeneo ya mjini.

Hata hivyo Mhandisi Seff aliwataka wananchi wa mji wa Kilosa kuunda vikundi vya kijamii kwa ajili ya kufanya kazi za kusafisha barabara na mifereji ili waweze kutunza miundombinu wanayojengewa na Serikali lakini pia kuwaongezea vipato na kuondokana na umaskini.

Naye, Diwani wa Kata ya Mbuni Shabani Maringo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa ujenzi wa mifereji ya maji katika mji wa Kilosa ambayo imepunguza madhara ya mafuriko kwa kiasi kikubwa katika mtaa wa Viwandani,Madaraka, Mjini, Makaburini na Shule ya Msingi Kichangani.

Amesema athari wanazopata sasa zinatokana na maji yaliyoelekezwa kutoka kwenye matoleo ya maji ya mradi wa SGR na kuiomba TARURA kujenga mifereji mingine ili kuyachepusha maji hayo yanayozidi kwenye mfereji wa awali pamoja na kumalizia ujenzi wa mfereji wenye urefu wa mita 750 uliochimbwa kwa nguvu za wananchi.

Previous articleWAZIRI MAKAMBA KUMWAKILISHA MHE RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA NNE WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA ITALIA
Next articleMELI 13 ZINAHUDUMIWA MUDA HUU BANDARI YA DSM JANUARI 28/2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here