Home LOCAL MAKONDA AWAVAA CHADEMA, ASEMA WAMEZOEA LUHARIBU UTARATIBU NA KUPOTOSHA

MAKONDA AWAVAA CHADEMA, ASEMA WAMEZOEA LUHARIBU UTARATIBU NA KUPOTOSHA

 

 

 

Awajibu kwa hoja upotoshaji wao unaolenga kumtweza Rais Samia na kudhalilisha Watanzania

Amjibu Mbowe asitumie agenda ya maandamano uchaguzi wao 

Awataka Mbowe, Lissu na Mnyika kwenye mdahalo kabla ya maandamano

Ampongeza Lissu kupuuza maandamano, kwenda AfCON

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Paul Makonda ‘amemvaa’ Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akimtaka aache kuendeleza tabia ya upotoshaji kama kete yake kubwa ya kufanya siasa nchini. 

Makonda amesema kuwa chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Watanzania wameshuhudia haki ikisimamiwa kikamilifu, ikiwa ni pamoja na jitihada mbalimbali binafsi za Mheshimiwa Rais alizozifanya katika kuunda Tume ya Haki Jinai, kupitia mambo kadha wa kadhaa ili kuhakikisha kwamba Mtanzania anapata haki yake bila kujali rika, elimu kipato, kabila , dini na hata kule alipotokea. 

Ndugu Makonda ameyasema hayo Jumapili Januari 14, 2024, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mjini Zanzibar, kuhusu hoja mbalimbali dhidi ya upotoshaji uliofanywa na Chadema, kupitia kwa Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, alipozungumza na waandishi wa habari jana Jumamosi. 

“Kwa masikitiko makubwa jana tumepata nafasi ya kumsikia kaka yetu Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA akituhumu na kutoa kauli za kuzalilisha na kufedheesha na kutweza utu wa Kiongozi wetu bila kujali dhamira njema aliyoonyesha Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa Umoja na Mshikamano katika Taifa letu”

“Taifa hili kwa mara ya kwanza limeshuhudia haki ikisimamiwa kikamilifu ikiwa pamoja na jitihada binafsi za Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais wa Tanzania alizozifanya katika kuunda Tume ya Haki jinai kupitia mambo kadhaa wa kadhaa ili kuhakikisha kwamba Mtanzania anapata haki yake bila kujali rika, elimu kipato, kabila , dini na hata kule alipotokea.”

“Mbowe kasema maneno mazito sana, upo wakati tumetafakari ya kwamba hakuna sababu ya kumjibu lakini imefika wakati tukasema Hapana…kwanini tumuache apotoshe umma kwa kichecheo ambacho hatuelewi msingi wake ni nini?,” amesema Ndugu Makonda na kuongeza;

“Moja ya hoja kubwa aliyosimama nayo katika mchakato huu wa mswaada wa sheria tatu (Sheria ya vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi yenyewe) amediriki kusema hadharani ya kwamba mapendekezo yaliyotolewa na kikosi kazi kilichoundwa na Mhe. Rais kwa mapenzi mema , mapendekezo yaliyotolewa na CCT pamoja na mapendekezo yaliyotolewa na baadhi ya vyama vya siasa kwamba yote yamepuuzwa …jambo hilo sio kweli hata kidogo”

“Mbowe anafahamu katika mapendekezo 84 yaliyotolewa mapendekezo 63 yote yamechukuliwa na yapo kwenye msawaada ambao hatua za kisheria zinaendelea katika kuunda kwa sheria na yeye ni mnufaika mkubwa wa maridhiano ambayo yamemfanya akawa yupo huru na kesi zote za kisiasa kuachiwa huru bila masharti na yeye mwenyewe na chama chake na vingine kufanya mikutano ya hadhara bila kubugudhiwa tena kwa mlinzi mkali chini ya Jeshi la Polisi kuhkikisha dhamira ya Rais Samia inatimia si tu kwa vyama vya siasa bali kwa Watanzania wote.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here