TMDA
Home LOCAL MAJALIWA AHUDHURIA MKUTANO WA G77 NA CHINA, KAMPALA, UGANDA

MAJALIWA AHUDHURIA MKUTANO WA G77 NA CHINA, KAMPALA, UGANDA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 21, 2024 amehudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77na China uliofanyika jijini Kampala nchini Uganda.

Katika Mkutano huo, Rais wa Uganda Yowezi Kaguta Museveni alikabidhiwa uenyekiti wa kundi hilo la G77 na China kutoka kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdés Mesa.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa uenyekiti Rais Museveni amesisitiza umuhimu wa umoja kati ya wanachama wa G77 na China katika kushughulikia changamoto za kidunia na kutoa wito kwa mataifa yanayoendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo za nchi zinazoendelea.

G-77 na China ni umoja ilioanza kama kundi la nchi 77 zinazoendelea ambazo zilikutana na kutia saini tamko la pamoja la mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo (UNCTAD) huko Geneva mwaka 1964, kwa lengo kuu la kukuza ushirikiano wa kiuchumi. miongoni mwa nchi wanachama wake na kushughulikia kwa pamoja masuala yanayohusu maendeleo, biashara na taasisi za fedha za kimataifa.

Mheshimiwa Majaliwa amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo wa siku mbili ambao umeanza leo Januari 21, 2024 na kutarajiwa kumalizika kesho Januari 22, 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea MAJALIWA AHUDHURIA MKUTANO WA G77 NA CHINA, KAMPALA, UGANDA