Home BUSINESS KAMISHNA WA TAWA AZINDUA MRADI WA JENGO LA OFISI LENYE THAMANI YA...

KAMISHNA WA TAWA AZINDUA MRADI WA JENGO LA OFISI LENYE THAMANI YA ZAIDI YA TZS MILIONI 250, AMPONGEZA RAIS SAMIA

Na: Mwandishi wetu, Kigoma

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Nyanda amezindua mradi wa jengo la ofisi lenye jumla ya vyumba 8 vikiwemo vyumba 6 vitakavyotumika kama ofisi, chumba cha mikutano, stoo pamoja na vyoo viwili, mradi unaotajwa kugharimu zaidi ya Tsh. Millioni 250.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo iliyofanyika leo Januari 16, 2024 Makao Makuu ya Ofisi za Pori la Akiba Moyowosi zilizopo Kifura wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mabula amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha taasisi hiyo kukamilisha mradi huo na miradi mingine ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa TAWA.

“Tunamshukuru Dk. Samia amefanya kazi nzuri ya kutupatia fedha zilizotuwezesha kukamilisha mradi huu na miradi mingine tunayoitekeleza ikiwa ni pamoja na mishahara, yote hii ni matokeo ya Serikali yetu, ndiyo inayotuwezesha,” amesema Kamishna Mabula.

Aidha amewataka wahifadhi wa Pori la Akiba Moyowosi kuhakikisha wanalitunza vizuri jengo hilo ikiwa na pamoja na kuimarisha usimamizi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na TAWA ndani ya hifadhi hiyo.

Katika hatua nyingine, Kamishna huyo ameupongeza uongozi wa Pori hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kulinda rasilimali walizopewa kusimamia kiasi cha kuwavutia wawekezaji.

“Nimefarijika sana wakati napokea taarifa yenu kujulishwa kwamba Pori la Akiba Moyowosi lina vitalu vya uwindaji wa kitalii 6 , na kati ya vitalu hivyo 6 vitano vina wawekezaji,” amesema.

“Niseme tu kwamba hawa wawekezaji hawajaja bure wamekuja hapa kwasababu kuna rasilimali na hii rasilimali ipo kwasababu ya kazi yenu nzuri, mmefanya kazi nzuri ya kuhakikisha wanyama walioko kule porini na mazingira yao yako salama..kwahiyo niwapongeze sana kwa hilo” ameongeza.

Kwa upande wake Kamanda wa Pori la Akiba Moyowosi David Mnyapwani ameipongeza Serikali kupitia Menejimenti ya TAWA kwa jitihada za dhati za kuwezesha miradi inayotekelezwa katika Hifadhi hiyo kujengwa na kukamilika kwa wakati

Ujenzi wa mradi huo ulianza kutekelezwa Mei 5, 2023 na kukamilika Septemba 9, 2023 na tayari umeanza kutumika…

Previous articleMRADI WA UBORESHAJI USALAMA WA MILKI ZA ARDHI WACHANGIA ONGEZEKO LA WANAWAKE KUMILIKI ARDHI NCHINI
Next articleRAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here