Wenyeji wa mashindano ya AFCON 2024 timu ya Taifa ya Ivory Coast imeanza vema michuano hiyo kwa kuichapa timu ya Taifa ya Guinea Bissau magoli 2-0.
Huo ni mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa michuano hiyo inayofanyika nchini Ivory Coast ikiwa na michezo 53 itakayopigwa katika viwanja tofauti nchini humo.
#Afcon2024