Home SPORTS IVORY COAST 0-1 NIGERIA, AFCON

IVORY COAST 0-1 NIGERIA, AFCON

Wenyeji wa Michuano ya AFCON timu ya Taifa ya Ivory Coast imepokea kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa mzunguuko wa pili wa kundi A uliopigwa Jijini Abidjan nchini humo.

Goli la Nigeria lilipatikana kwa mkwaju wa penati na Nahodha wake Wiliiam Ekong katika Dakika ya 55 ya kipindi cha pili cha mtanange huo.

Wenyeji Ivory Coast waliongeza kasi kutaka kusawazisha goli hilo, lakini juhudi zao ziliendelea kufifia huku dakika zikiyoyoma bila mafanikio, hadi mwisho wa mchezo huo.

Kufuatia matokeo hayo, imewawezesha Equatorial Guinea kukaa kileleni mwa kundi A, ikiwa na alama 4 baada ya kuichapa Guinea Bissau magoli 4-2, ikifuatiwa na Nigeria mwenye alama 4, huku Ivory Coast wakiwa nafasi ya 3 na alama 3, na wa mwisho ni Guinea Bissau akiwa na alama 0.

#afcon
#Afcon2024
#ivorycoast🇨🇮
#soccernigeria
#drogbalegend
#okocha
#soccerafrica

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here