Timu ya Taifa ya Misri imetoka sare ya magoli 2 -2 na timu ya Taifa ya Ghana katika mchezo wa mzunguuko wa pili mashindano ya AFCON yanayotimua vumbi nchini Ivory Coast.
Timu ya Ghana ndio ilikuwa ya kwanza kuzifumania nyavu za Misri katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza kupitia kwa kiungo mshambuliaji Mohamed Kudus, goli lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili Misri walionesha kujipanga na kucheza kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha likifungwa na mshambuliaji wake Omar Mormoush, katika dk ya 69 ya mchezo huo.
Iliwachua dakika 4 tu timu ya Ghana kupachika goli la pili likifungwa na Mohamed Kudus tena, akipiga shuti lililomshinda mlinda mlango wa Misri, dakika ya 71 ya mtanange huko. Hata hivyo, goli hilo lililodumu dakika 3 tu ambapo Misri walisawazisha kupitia kwa Mostafa Mohamed dk ya 74 ya mchezo huo, goli lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo.
Matokeo hayo yanaiweka njia panda Ghana wakishika mkia katika kundi B wakiwa na alama 1, huku Cape Verde wakiongoza kundi hilo wakiwa na alama 3.