Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi amewahakikishia Makatibu Wakuu wa Vyama Sita vya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika kwamba Chama Cha Mapinduzi kina uhakika wa kushinda kwa kishindo katika changuzi za mwaka huu na mwaka kesho, kwa maana ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.
Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita vya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika kilichofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyopo Kibaha mkoani Pwani.
Kauli hiyo aliitoa baada ya kuwapongeza Chama Cha ZANU – PF cha Zimbabwe Kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wao walioufanya huku akivitakia pia heri ya ushindi NAMIBIA NA AFRIKA KUSINI kwenye uchaguzi wao mkuu ambao wao wanaufanya baadae mwaka huu na ANC cha Afrika kusini ambacho kimesheherekea kumbukumbu ya miaka 112 tangu kuanzishwa kwake.

Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Kusini, wakiwa katika picha ya pamoja, wakati walipokutana kwa ajili ya kikao cha kazi, kujadili agenda mbalimbali katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) iliyopo Kibaha, mkoani Pwani. Kutoka kulia ni Komredi Obert Moses Mpofu, Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU- PF (Zimbabwe), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM (mwenye shati ya kijani), Komredi Sophia Shaningwa Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia), Komredi Francisco Mucanheia ambaye ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Komredi Manuel Domingos Augusto, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa MPLA (Angola) na mwishoni kushoto ni Komredi Fikile Mbalula, Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini)