Home BUSINESS Dkt. KUSILUKA SERIKALI ITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO UJENZI KONGANI YA VIWANDA, KWALA

Dkt. KUSILUKA SERIKALI ITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO UJENZI KONGANI YA VIWANDA, KWALA

Suzanianism PR Viwanda: Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi . Dkt. Moses Kusiluka akiwa pamoja naWaziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji, Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba wakiangakia bidhaa za urembo na nguo zinazotengenezwa na moja ya viwanda katika Mradi Mkubwa wa Viwanda zaidi ya 200 unaoendelea kutekelezwa katika eneo la Kwala Kibaha Mkoani Pwani Januari 5, 2024.

Suzanianism PR Viwanda: Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Balozi Dkt. Moses Kusiluka akiongozana na Mawaziri akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali wakiwemo Makatibu Wakuu katika ziara ya kukagua Maendeleo wa Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Viwanda zaidi ya 200 unaoendelea kutekelezwa katika eneo la Kwala Kibaha Mkoani Pwani Januari 5, 2024.

PWANI, Januari 5, 2024

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi . Dkt. Moses Kusiluka amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Viwanda zaidi ya 200 unaoendelea kutekelezwa katika eneo la Kwala Kibaha Mkoani Pwani.

Katibu Mkuu Kiongozi Kusiluka ameyasema hayo Januari 5,2024 akiongozana na Mawaziri na Wakuu wa Taasisi mbalimbali katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo unaotarajiwa kuwa na viwanda zaidi ya 200 uliopo katika eneo la Kwala Mkoani Pwani.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji na itahakikisha Mradi huo muhimu na wenye faida nyingi hususani katika kuongeza ajira, Pato la Taifa na ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa ujumla unakamilika.

Kwa upande wa Waziri wa Viwanda na Biashara Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji ameseam Mradi huu unaojumuisha viwanda zaidi ya 200 utakapokamilika utatoa ajira zaidi ya laki moja na vijana wengi kutoka ndani ya Mkoa wa Pwani na Taifa kwa ujumla watapata ajira hali itakayoimarisha uchumi wa Taifa kwa ujumla

“Zaidi ya Asilimia 90 ya mabinti ambao tuliowaona katika kile kiwanda cha kutengeneza nguo wanatoka hapa Kwala na waliniambia kabisa kuwa walitembea mitaani kwetu na kuweza kuwachukua wadada kila aliekuwa na cherehani yake nyumbani na kuanza nao hapa na wengine wanakuja”. Amesema Kijaji.

Aidha Dkt Kijaji alibainisha kuwa katika ziara hiyo walitembelea viwanda viwili kati ya 200 na kimoja wapo ni cha kutengeneza nguo [vijora] zinatumika ndani ya Tanzania na vinasambazwa Dubai ambapo bidhaa hizo zinachangia upatikanaji wa fedha za kigeni kutokana na uwekezaji unaoendelea. 

Previous articleMAJALIWA: TUENDELEE KUPINGA UKATILI KWA WATOTO
Next articleTANZANIA INA UWEZO WA KUZALISHA NONDO NA MABATI KWA SOKO LA NDANI NA NJE 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here