Home BUSINESS BoT KUANZA KUTEKELEZA SERA MPYA YA FEDHA JANUARI 2024

BoT KUANZA KUTEKELEZA SERA MPYA YA FEDHA JANUARI 2024

Wahariri na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango wakati akitoa mada kuhusu utekelezaji wa sera mpya ya fedha katika semina iliyofanyika ukumbi wa BoT Januari 9,2024 Jijini Dar es Salaam.

Meneja Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Vick Msina akiwa pamoja na Mchumi Mkuu Mwandamizi Kurugenzi za Sera, Uchumi na Utafiti Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Lusajo Mwamkemwa kushoto katika semina hiyo, Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahariri  wa habari wakifuatilia wasilisho la Sera mpya ya fedha inayotarajiwa kuanza kutekelezwa na Benki Kuu ya Tanzania BoT.

Afisa Mawasiliano Mwandamizi  Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Bw. Lwaga Mwambande  akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM 

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeanza kutekeleza sera mpya ya fedha ili kuongeza ufanisi katika kudhibiti mfumuko wa bei pamoja na kuimarisha shughuli za uchumi.

Hayo yamebainishwa na  Mchumi Mkuu Mwandamizi na Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Sera, Uchumi na Utafiti Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Lusajo Mwamkemwa  katika mahojiano na waandishi wa habari wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari,  iliyofanyika Januari 9,2024 Jijini Dar es Salaam.

Mwamkemwa, amesema kuwa mabadiliko hayo yanaendana na makubaliano ya kutumia mfumo mmoja wa utekelezaji wa sera ya fedha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

amesema kuwa Tanzania imechelewa kutekeleza sera hiyo kutokana kwamba walikuwa wanafanya maandalizi ya kutosha ili kutengeneza mazingira rafiki.

“Mfumo huu sio mpya Duniani na sisi Tanzania tunaingia sasa baada ya kujiridhisha kwa kufanya maandalizi ya kutosha, nchi zote za Afrika Mashariki zinaingia katika utekelezaji wa sera hii ili kuwa na ulinganisho” Bw.Mwamkemwa

Kwa upande wake Mkurugenzi wa utafiti na Sera za Uchumi BoT Dkt. Suleiman Missango, akizungumza alipokuwa akitoa mada katika semina hiyo, amesema kuwa sera mpya ya fedha itatumia mfumo wa riba hatua ambayo itasaidia kudhibiti mfumuko wa bei na kuwezesha ukuaji wa uchumi.

“Riba hii itajulikana kama Riba ya Benki itakayotumika kama kigezo cha kuweka viwango vya riba kwa wateja wa Benki na taasisi nyingine za fedha” amesema Dkt. Missango.

Semina hiyo ya siku moja kwa Wahariri na Waandishi wa habari imelenga kutoa uelewa mpana kwa wadau hao kwani wana jukumu kubwa la kutoa elimu kuhusu sera hiyo ambayo itaanza kutekelezwa  mwezi Junuari, 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here