Home LOCAL JNHPP YAWA KIVUTIO ZANZIBAR

JNHPP YAWA KIVUTIO ZANZIBAR

*Wajiuliza mradi umefanikiwa vipi?
*Wakusanyika kupiga picha kwenye Bango

Na Mwandishi wetu Zanzibar

Watu wengi Mjini Unguja,Zanzibar wamejitokeza kutembelea Banda la TANESCO katika viwanja vya Fumba ambapo Maonesho ya 10 ya kimatafa ya Biashara yanafanyika .

Maonesho hayo yaliyoanza 7 January 2024, yameleta Taswira mpya ya wadau wa Umeme juu ya jitihada ambazo Serikali inazifanya kwenye uwekezaji wa Sekta ya Nishati Nchini.

Mmoja ya wadau aliyetembelea Banda hilo ni Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Selestine Kakele ambae ameonekana kuvutiwa na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) na hasa mradi wa JNHPP ambao umefikia asilimia 95.83

Naye Mwangulumba Mtumishi katika Bodi ya Taifa ya Pamba Nchini amesema kuwa mradi wa JNHPP ni tumaini jipya kwa Tanzania na kuwa utekelezaji wake umekua wa kipekee sana kwani ni mradi uliopitia changamoto nyingi sana hasa kutoka katika Mataifa makubwa yaliyoendelea lakini Tanzania imeonesha uthubutu.

“Najiuliza tumewezaje kulifanya hili, huu mradi wa kipekee , maono ya waasisi wetu yalikua makubwa sasa hata wale ma Giant wanatushangaa, hili tumeliweza,” amesema.

Kwa upande wake Issa Waziri mkazi wa Pemba, amesema kuwa mradi wa JNHPP si tu utawapatia umeme wa kutosha lakini umekuwa kivutio kwa namna unavyoonekana.

Shamra shamra za Maonesho haya zimekua za kihistoria kwa TANESCO na hasa kwa baadhi ya watu kuja na kupiga picha katika moja ya bango la Mradi wa JNHPP.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here