Home SPORTS YANGA SC YAPATA ALAMA MOJA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

YANGA SC YAPATA ALAMA MOJA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Timu ya wananchi, Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC imeshindwa kufua Dafu kwenye ikiwa  nyumbani kwa kitoka sare ya 1-1 na timu ya Alhly ya Misri kwenye mchezo wake wa pili wa ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa katika Dimba la Mkapa Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza timu zote mbili zilienda mapumziko bila kufungana na kipindi cha pili kilianza kwa kila mmoja kufanya mabadiliko.
Al Ahly walipata bao dakika ya 86 likifungwa na Percy Muzi Tau huku watu wakiamini Yanga hawezi kurudisha bao kutokana na dakika kuwa ukingoni alikuwa kiungo  Fundi kutoka Ivory Coast, Pacôme Zouzoua aliisawazisha Yanga dakika ya 90 +1.
 
Kwa Matokeo hayo Al Ahly imefikisha pointi nne na kuendelea kuongoza Kundi D kwa pointi moja zaidi ya wote, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia baada ya mechi mbili.
 
Mechi inafuata Yanga SC itasafiri hadi nchini Ghana kucheza na Medeam  Ijumaa ya Desemba 8, wakati Al Ahly watawakaribisha CR Belouizdad Jijini Cairo.
Previous articleMAJALIWA AIPONGEZA GGML MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI,MAAMBUKIZI MAPYA YASHUKA
Next articleWAZIRI MKUU AKABIDHI VITI VYA MAGURUDUMU KWA WATU WENYE ULEMAVU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here