Mamlaka ya USafiri wa Anga nchini imeratibu zoezi la kuwaaga washindi watano wa mbio za kujifurahisha (FUN RUN) zilizofanyika Oktoba 29 jijini Dar es salaam zikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuundwa kwa TCAA.
Washindi hao walipata zawadi za tikteki kutoka kwa wadau wa Usafiri wa Anga ambao ni mashirika ya ndege ya Ethiopian Airlines, Kenya Airways na Fly Dubai ambapo wataelekea Dubai kwa mapumziko ya siku tano.
Akizungumza wakati wa kuwaaga, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA ambaye pia ni Meneja Mipango wa Mamlaka hiyo Bi. Mellania Kasese aliwapongeza washindi hao na kuyashukuru Mashirika yaliyotoa tiketi hizo kwa kutimiza ahadi hiyo na kuishukuru TCAA kwa kugharamia fedha za kujikimu kwa washindi hao wawapo katika mapumziko hayo.
“Ni siku ya sote kufurahia utimilifu wa zoezi hili kwa washindi wetu hawa watano ambao walipatikana miongoni mwa zaidi ya washiriki 300. Nawatakia safari njema na hii iendelee kuwa chachu ya kujali afya zenu lakini ikawe hamasa kwa wengine ili wajikite katika kuimarisha afya zao kwa mazoezi,” amesema Mellania.
Meneja wa Shirika la Ndege la Ethiopia Bi. Seble Woldemariam amewapongeza washindi na kuwataka kutumia fursa hii kufanya utalii na kujifunza mengi mema na mazuri watakayojionea huko waendako..
Meneja Mipango TCAA Melania Kasese akizungumza na wanahabari wakati wa tukio la kuwaaga washindi wa TCAA FUN RUN waliojishindia tiketi za kuelekea Dubai ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Bw. Samuel Makalla mtumishi wa TCAA akielezea maandalizi aliyofanya kuelekea safari ya Dubai mara baada kuibuka mshindi wa TCAA FUN RUN kwenye Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Mtumishi wa TCAA Bw. Aidan Adrian ambaye ni miongoni mwa washindi akitoa shukrani kwa wote waliofanikisha zoezi hilo wakati TCAA FUN RUN iliyofanyika katika maadhimisho ya Miaka 20 ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) iliyopelekea kutangazwa mshindi wa mashindano hayo.
Mtumishi wa LATRA Bw. Lugano Mwasomola ambaye ni miongoni mwa washindi akitoa shukrani kwa wote waliofanikisha zoezi hilo pamoja nasafari hiyo ya kwenda Dubai wakati wa hafla ya kuondoka hapa nchini kuelekea Dubai.
Meneja wa Shirika la Ndege la Ethiopia Bi. Seble Woldemariam (katikati) akizungumza wakati wa kuwaaga washindi wa tiketi ya kuelekea Dubai ambapo Shirika hilo ni miongoni mwa wadau waliotoa tiketi moja wapo kwa mshindi.
Meneja Mipango kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Melania Kasese akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa tiketi ya kuelekea Dubai pamoja na viongozi wa Shirika la Ndege la Ethiopia pamoja na Emirate wakati wa kuondoka nchini kwa ajili ya kwenda kutembea Dubai.