Home SPORTS SIMBA SC YAAMBULIA SULUHU YA 0-0 UGENINI

SIMBA SC YAAMBULIA SULUHU YA 0-0 UGENINI

TIMU ya Simba SC wameshindwa kutamba ugenini katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kulazimishwa sare bila kufungana dhidi ya wenyeji,  Jwaneng Galaxy  mchezo wa Kundi B uliopigwa  Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana.
 
Licha ya kutawala mchezo Simba SC  walishindwa kutumia nafasi walizozipata kutoka kwa wenyeji hao huku wakiwa na Kocha wao Mpya  Mualgeria Abdelhak Benchikha.
Kwa matokeo hayo Simba wamefikisha pointi mbili baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast huku  Jwaneg Galaxy wanafikisha pointi nne baada ya kuanza na ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Wydad Athletic Jijini Marrakech wiki iliyopita.
Simba SC itashuka uwanjani Desemba 9 kucheza na wenyeji Wydad Casablanca nchini Morocco,huku Jwaneng watakuwa wenyeji dhidi ya ASEC Mimosas  hapo hapo Francistown. 
Previous articleSOMA HABARI MAGAZETI YA LEO DISEMBA 2-2023
Next articleMAJALIWA AIPONGEZA GGML MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI,MAAMBUKIZI MAPYA YASHUKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here