Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Simon akitoa wasilisho katika kikao kazi kilichowakutanisha Wahariri wa Habari nchini, na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), kilichofanyika leo Disemba 11,2023 Jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabatho Kosuri akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi katika kikao kazi kilichowakutanisha Wahariri wa Habari nchini na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), kilichofanyika leo Disemba 11,2023 Jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo , DAR
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeokoa zaidi ya Shillingi Bilioni 500 kutokana na uwepo wa mfumo wa uagizaji Mafuta kwa pamoja.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Simon alipokuwa akotoa mada juu ya namna Taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu kwa mujibu waSheria katika kikao kazi kilichowakutanisha Wahariri wa Habari nchini na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), kilichofanyika leo Disemba 11,2023 Jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nishati ya mafuta inapatikana wakati wote na kwa bei nafuu .
“Katika kutekeleza hili, Serikali ya Awamu ya Sita imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa ruzuku kwenye gharama ya mafuta kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai, 2022 hadi Disemba, 2022 ill kupunguza bei ya mafuta kwa wananchi na kuwa stahimilivu” amesema Simon.
Ameeleza kuwa Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekuwa ikitoa kiasi cha fedha cha Dola za Marekani kwa Benki za Biashara ili ziweze kulipia mafuta yanayotumika nchini.
Sambamba na hilo ameeleza kuwa Serikali kupitia Benki Kuu ilibadilisha baadhi ya miongozo ya udhibiti wa Dola za Marekani ili kuwezesha Benki za Biashara kupata fedha hizo kutoka sokoni.
PICHA NA: HUGHES DUGILO)