Home BUSINESS OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YANG’ARA TUZO ZA NBAA

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YANG’ARA TUZO ZA NBAA

Mkurugenzi wa usimamizi wa Utendaji, Ufuatiliaji na Tathmini – Mashirika ya Kibiashara, Bi. Lightness Mauki (kulia), akipokea tuzo kutoka  kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, CPA Jamal Kassim Ally (kushoto) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo zilizondaliwa na Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. (wa pili kulia). ni Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu wa Taasisi hiyo Hassan Mohamed.

DAR ES SALAAM 

Ofisi ya Msajili wa Hazina imeng’ara kwa kuibuka mshindi wa kwanza katika tuzo za uandaaji wa taarifa za fedha kwa mwaka 2023 katika kundi la Idara Huru za Serikali (Independent Government Department).

Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki na Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika hafla iliyofanyika mwisho mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

Ofisi ya Msajili wa Hazina iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Usimamizi, wa Utendaji, Ufuatiliaji na Tathmini – Mashirika ya Kibiashara, Bi. Lightness Mauki akiambatana na Mkurugenzi wa Fedha na Uhasibu wa Taasisi hiyo Hassan Mohamed, kwa niaba ya Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Bi. Mauki amesema kuwa ushindi walioupata utaongeza chachu ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuimarisha utendaji kazi katika Taasisi yao.

Bodi ya Taifa ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kutoa tuzo kwa Mashirika na Taasisi za Serikali zilizofanya vizuri  kutambua kazi wanazofanya.

Previous articleWAHITIMU CHUO CHA BIBLIA MUWE MABALOZI WAZURI KWA KUSIMAMIA MAADILI WAZIRI MHAGAMA
Next articleRAIS SAMIA AKUTANA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MICHAEL BLOOMBERG ,KANDO YA MKUTANO WA COP28, DUBAI, UAE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here