Home LOCAL NCHI 56 KUSHIRIKI MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIA NCHI

NCHI 56 KUSHIRIKI MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Na Avila batwely Greenwaves media

kampuni na Taasisi 56 zimeonesha nia ya kuwekeza nchini kwa kushirikiana na sekta binafsi kupitia mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (Cop28) na Tanzania itanufaika na fedha za miradi.

Mkutano huo uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 12 mwaka huu wenye lengo la kupitia taarifa, kufanya kutatmini, majadiliano na maamuzi kuhusu hatua zilizochukuliwa nan chi wanachama katika kufikia malengo ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi.

Hayo ameyasema leo Disemba 18 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk.Seleman Jafo wakati akitoa taarifa kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi (Cop28).

Amesema Tanzania inapoteza asilimia 2 hadi 3 ya pato la Taifa kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi.

kampuni na Taasisi 56 zimeonesha nia ya kuwekeza nchini kwa kushirikiana na sekta binafsi kupitia mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (Cop28).

“Wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania walikutana na wawekezaji kutoka nje ya nchi na kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji kwenye eneo la mabadiliko ya Tabia ya Nchi ambapo jumla ya taasisi na kampuni zaidi ya 56 zimeonesha nia ya kuwekeza nchini kwa kushirikiana na sekta binafsi nchini,”amesema Dk. Jafo.

Ameeleza kuwa kupitia Mkutano wa 28 Tanzania itanufaika zaidi na fedha za miradi, teknolojia, utaalam na Programu mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo Programu ya Afrika ya Nishati Safi ya Kupikia; programu ya Afya na mabadiliko ya Tabia ya Nchi; na utekelezaji wa mikakati ya kuimarisha uhimili katika katika sekta ya maji, misitu na Bahari.

Amesema Tanzania imeshiriki mikutano ya pembezoni ya ngazi ya juu iliyohusu uzinduzi wa Mpango wa kukuza matumizi na nishati safi na nafuu ya kupikia kwa wanawake barani Afrika ulioshirikisha wadau ana kwa ana 150.

“Pia kulikuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu fursa za uwekezaji kwenye sekta ya kilimo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi , mkutano wa kuongeza kasi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi katika sekta ya kilimo kwa kushughulikia hasara na uharibifu unaotokana na athari mabadiliko ya tabia nchi ,”amesema.

Amesema masuala yaliyojadiliwa katika Mkutano huo ni mikakati ya kukusanya Dola za Marekani bil 1.8 kwa ajili ya kuchimba visima 65,000 ambapo kila kisima kimoja kitahudumia wakulima wenye mashamba ya ukubwa wa hekta 2.5.

“Wadau wa Maendeleo waliahidi kuchangia programu hii kiasi cha Dola za Marekani Mil 610,”amesema.

Dk.Jafo ametaja wadau walioahidi kuchangia ni World Bank USD Milioni 300; Africa Development Bank (AfDB) USD Milioni 100, AGRA USD Milioni 50, IFAD USD Milioni 60, USAID USD Milioni 100, AfDB imekubali kuwa mtafutaji fedha kuhakikisha upatikanaji wa fedha za uchimbaji wa visima 65,000.

Amesema programu hiyo itasaidia uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya Kilimo na itapunguza uharibifu wa mazingira.

Dk.Jafo amesema katika Mkutano huo sekta binafsi na Asasi za Kiraia (AZAKI) 340 zilishiriki ipasavyo katika mkutano wa COP28 ikiwemo banki ya Kilimo ya Taifa ambazo zilikuwa sehemu kubwa ya wajumbe wa Tanzania walioshiriki katika mkutano huo.

Alifafanua kuwa katika mkutano huo nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa mabadiliko ya Tabia nchi zilikuwa na makubaliano 11 ambayo lengo la pamoja la kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi.
Pia uendeshaji wa Mfuko wa kukabiliana na upotevu na uharibifu utokanao na mabadiliko ya tabianchi pamoja na uundwaji wa Bodi ya ushauri ya Mfuko huo.

Aidha amesema mkutano wa 29 COP29 kufanyika Azerbaijan Novemba 11 hadi 22 mwaka 2024 na mkutano wa 30 unatarajia kufanyaka nchini Brazil Novemba 10 hadi 21 mwaka 2025.

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here