Home SPORTS YANGA SC YAICHARAZA SIMBA 5-1 KARIAKOO DERBY KWA MKAPA

YANGA SC YAICHARAZA SIMBA 5-1 KARIAKOO DERBY KWA MKAPA

Mchezo wa Dakika 90 ambazo zimechezwa katika uwanja wa Mkapa jijini Dar-es-Salaam kati ya timu ya Simba  SC na Yanga SC zimemalizika ikiwa Yanga SC imeicharaza Simba SC kwa  ushindi wa bao 5 – 1  za Mchezo huo wa Kariakoo Dabi 

Kipindi cha pili Yanga walionyesha wanahitaji ushindi na kufunga mabao kupitia kwa Maxi Nzengeli ambaye alifunga mawili dakika ya 64, 77, Aziz KI dakika ya 73, Pacome bao la tano dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti.

Ndani ya dakika 45 za mwanzo ilikuwa ni sambamba kwa Simba 1-1 Yanga.

Bao la Yanga lilifungwa dakika ya tatu na Kennedy Musonda na bao la Simba limefungwa na Kibu Dennis dakika ya 8.

Hivyo kuifanya timu ya Yanga SC kuibuka kidedea kwa mchezo huu na kuwaziba midomo mashabiki wa Simba SC

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here