Na: Mwandishi wetu
Wadau mbalimbali nchini wamekutana kujadili na kutoa mapendekezo ya kuboresha mapitio ya mitaala ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na kutoa maoni ya uanzishwaji wa kampasi ya Chuo hicho Mkoani Kigoma.
Akizungumza Leo Novemba 6 Jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Kenneth Hosea wakati akifungua mkutano wadau mbalimbali ambao utudumu kwa siku mbili.
Amesema shughuli hizo mbili zipo ndani ya maeneo nane ya mradi wa elimu ya juu kwa mabadiliko ya uchumi (HEET) ambao ni mageuzi ya elimu ya juu kwa maendeleo ya uchumi hususani katika sekta ya afya.
” Siku hii ni muhimu yenye maan kubwa kufungua mkutano huu muhimu wa wadau ili kujadili mapitio ya mitaala katika jitihada za kuleta mabadiliko ya elimu yetu ya juu kwaajili ya kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini, “amesema Dk. Hosea.
Amesema mabadiliko ya elimu ya juu ni yenye kulenga taasisi maalum kama MUHAS yanahitaji ushirikiano mpana na makini wa wadau ili kuhakikisha kwa mapitio ya mitaala yanashughulikia changamoto kubwa za rasilimali watu katika sekta zinakabili Taifa.
Amesema anatambua kuwa kama nchi wana changamoto na uhaba mkubwa ya rasilimali watu wa afya wenye ujuzi idadi na kwa ubora.
DK. Hosea amesema hivyo lengo mojawapo la mradi wa HEET hapo MUHAS ni kupitia mitaala upya yote ya uzamili na kubuni mitaala mipya kulingana na mahitaji ya nchi.
Ameeleza kuwa jumla ya mitaala 79 ya uzamili imepitiwa upya na mitaala 22 imeanzishwa katika shahada za awali na uzamili kupitia mradi wa HEET.
‘Jumla ya mitaala 16 ya shahada za uzamili zimianzishwa ambapo mitaala mitatu imeshapata ithibati kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) na inaanza kutumika mwaka huu na mitaala ya 13 itajadiliwa kwenye mkutano huu,”ameeleza.
Aidha amesema katika mkutano huo mitaala yote hiyo itajadiliwa na wadau ili kuweza kutoa maoni ya maboresho ili kuweza kutumika baada ya kujumuisha maoni na shauri utakaopatikana na hiyo ni awamu ya tatu ukusanyaji maoni kutoka kwa wadau.
Naye Naibu Makamu Mkuu wa MUHAS, Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema mwaka huu wana adhimisha miaka 60 tangu kwa kuanzishwa chuo hicho ikiwa lengo ni kuongeza idadi ya watumishi wa afya.
“Ushiriki wa wadau ni sehemu muhimu ya mitaala ya elimu ya juu ushiriki huu tunahakikisha kwa matokeo ya mafunzo na ujuzi ambao wanafunzi wamepata unawiana na mahitaji ya sasa na ya baadaye ya waajiri na jamii,” amesema Profesa Kamuhabwa.
Aidha amesema kwa kuhusisha wadau hawa katika mapitio ya mitaala taasisi za elimu ya juu zinaweza kuongeza umuhimu na ushawishi program zao na kutayarisha wahitimu wao kwa changamoto na fursa za karne ya 21 mbeleni.
Kwa upande wake Naibu wa Mradi wa HEET MUHAS, Dk. Nathanael Sirili amesema kupata maoni ya wadau ni muhimu hivyo ujenzi wa kampasi hiyo Ujiji mkoni Kigoma unatarajia kuanza mwakani utachukua mda wa miezi 24 hadi kukamilika.