Home LOCAL USCAF KUPELEKA MAWASILIANO KWA WANANCHI ZAIDI YA MILIONI 20 VINIJINI

USCAF KUPELEKA MAWASILIANO KWA WANANCHI ZAIDI YA MILIONI 20 VINIJINI

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina Thobias Makoba, akizungumza alipokuwa akitoa salamu za tangulizi katika kikao kazi kilichowakutanisha Wahariri wa Habari na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, kilichofanyika leo Octoba 21,2021 katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Justina Mashiba, akizungumza alipokuwa akiwasilisha mada katika kikao kazi hicho kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina , kilichofanyika Novemba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Albert Richard akitoa salamu zake katika kikao kazi hicho kilichofanyika leo Octoba 21,2023 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodaus Balile, akihutubia Mkutano huo na kutoa neno la Shukrani kwa niaba ya Wahariri wa Habari.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Anitha Mendoza, akiwa pamoja na Wahariri wengine wakifuatia hotuba na mada zilizokuwa zilizokuwa zikitolewa katika Mkutan huo.

DAR ES SALAAM.

Afisa Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF, Justina Mashiba, amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Mawasiliano itakayowezesha wananchi zaidi ya milioni 20 kupata huduma za Mawasiliano ya Simu kwa uhakika.

Amesema kuwa Serikali imewekeza kiasi cha shilingi Bilioni 326 kuwezesha ujenzi wa minara 2,149 na kwamba kukamilika kwa Mradi huo kutasaidia kufikisha Mawasiliano ya Simu vinijini.

Mashiba ameyasema hayo leo Novemba 21,2023 alipokuwa akitoa mada juu ya itekelezaji wa majukumu yao katika kikao kazi kati ya Mfuko huo na Wahariri wa Habari kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina Jijini Dar es Salaam.

“Serikali imeingia makubaliano ya Kimkakati na watoa huduma ya Mawasiliano ili kufikisha huduma hiyo kwenye kata 1,974 zenye Vijiji 5,111, ambapo mpaka sasa Jumla ya Kata 1,197 zenye Vijiji 3,613 vimefikiwa na huduma hiyo” amesema Mashiba.

Ameeleza kuwa uwekezaji huo uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mkubwa na kwamba umegusa na kunufaisha maeneo ya pembezoni mwa nchini.

Akizungumzia huduma hiyo kwa upande wa Zanizabar, Mashiba amesema kuwa hadi sasa imebaki sehemu chache kwa maeneo yote ya Zanizabar kifikiwa na huduma ya mawasiliano.

“Tunaendelea kuhakikisha njia zote ikiwemo barabara kuu zinakuwa na mawasiliano ili wananchi wote wapate mawasiliano”

Kikao Kazi hicho ni mwendelezo wa Mikutano inayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kuzikutanisha Taasisi za Umma na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kueleza shughuli wanazofanya katika kutekeleza majukumu yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here