Home BUSINESS UFANISI WA RAIS MWINYI WAONGEZA MAPATO ZRA

UFANISI WA RAIS MWINYI WAONGEZA MAPATO ZRA

Na: Halfan Abdulkadir ZANZIBAR

Miaka mitatu ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi, Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) imesema imeongeza ufanisi Mkubwa katika utendaji kazi wake

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Ndugu Yusuph Juma Mwenda wakati akiwasilisha mada katika Kongamano la kuadhimisha Miaka mitatu ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi lililoandaliwa na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, fedha na mipango Chini ya Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.l lililofanyika katika Ukumbi wa Michenzani Mall Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Amesema ndani ya Miaka mitatu ya Rais Mwinyi, Mamlaka ya Mapato ya Zanzibar (ZRA) imefanikiwa kujenga mifumo Rahisi na nafuu kwa ajili ya kuongeza ukusanyaji wa Kodi.

Kamishna Mwenda Ameitaja mifumo hiyo kuwa ni usawa katika kodi, uhakika wa kulipa kodi, urahisi wa kulipa Kodi sambamba na kuendelea kutoa elimu kwa walipa kodi ili kuendelea kufanyakazi kwa weledi na hatimaye kuweza kufikia lengo la ukusanyaji wa Kodi.

Mbali na hayo amewataka Wanafunzi kutoka Vyuo vikuu mbalimbali visiwani Zanzibar walioshiriki kongamano hilo kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha Wananchi kulipa kodi, hasa hasa katika kodi ya majengo ambayo ni kodi iliyokuwepo tangu zamani , lakini kwa sasa inakusanywa na (ZRA).

Kongamano hilo la kuadhimisha miaka mitatu ya Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi, lililoandaliwa na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango limeshirikisha Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Serikali ikiwemo ZRA, sambamba na Wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali Zanzibar.

Previous articleYANGA SC YAICHARAZA SIMBA 5-1 KARIAKOO DERBY KWA MKAPA
Next articleMAGAZETI YA LEO NOVEMBA 6-2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here