Home LOCAL SERIKALI YAIPA MENO MSD KUZALISHA VIWANDA VYA DAWA NA VIFAA TIBA

SERIKALI YAIPA MENO MSD KUZALISHA VIWANDA VYA DAWA NA VIFAA TIBA

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imewapa meno Bohari ya Dawa (MSD), katika uzalishaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.

Kutokana na hatua hiyo Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi ameitaka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), kukagua viwanda 12 vinavyozalisha bidhaa za afya ili kuiwezesha MSD kununua kwa wazalishaji hao.

Alisema hali hiyo itaiwezesha Serikali kuokoa sh bilioni 300 iwapo viwanda vya ndani vitazalisha bidhaa za afya.

Naye Mkurugenzi wa Tehama kutoka (MSD), Leopord Shao, alisema maamuzi hayo ya serikali ni muhimu kwa kuwa bajeti ya MSD kununua bidhaa za afya ni sh bilioni 590 kwa mwaka, lakini asilimia 80 ya fedha hizo sawa na sh. bilioni 300 inatumika kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi, huku kiasi kidogo ambacho ni sh. bilioni 100 ndiyo kinabaki ndani ya nchi.

Previous articleSERIKALI INATARAJIA KUANZA TATHMINI YA UJENZI WA UKUTA KATIKA FUKWE
Next articleTANZANIA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA HIARI KATIKA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here