Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA) kuhakikisha wanakwenda na kusimamia miradi yao kwa kuzingatia mda uliopangwa haiwezekani mradi wa mwaka moja mradi haujakamilika hilo jambo halikubaliki.
Kauli hiyo ameitoa leo Novemba 22 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri huyo alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo amesema Lengo kubwa kwenye ziara ya TCAA ni kufahamiana na kupata fursa ya kuonana na Menejimenti kiona wanafanya nini wana mipango gani? na mambo gani ya kuyapa kipaombele.
“Waendelee kusimamia ubora wa miradi hii iweze kukamilika kwa wakati na thamani ya fedha walizotoa waweke utaratibu mzuri wa kusimamia maelekezo yaliyotolewa na viongozi yawe na mfumo ya utekelezaji,” amesema Kihenzile.
Amesema pia waendelee kusimamia mashirika yetu ya ndege ya ndani na nje ili kudhibiti ajali na malalamiko ya wananchi ikiwa pamoja kuhairisha safari yaweze kutafutiwa ufumbuzi.
Amesema kazi ya huko inataswira mbili moja inaenda sambamba kurekebisha na kujenga viwanja vya ndege sehemu mbalimbali na TCAA wanasimamia ikiwemo Mtwara Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na vinginevyo.
“Zaidi ya mabilioni yameelekweza na bado Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatenga fedha ili kuhakikisha usalama wa vifaa vya mbalimbali vya angani ambavyo kimsingi vina dhibitiwa na vina simamiwa na TCAA,” amesema.
Aidha amesema ipo miradi kadhaa ambayo inafanyika mikubwa mojawapo ni ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga ambacho kinafanya kazi kufundisha watu mbalimbali.
“Tumeelezwa katika vyuo tisa Barani Afrika cha TCAA ni mojawapo na duniani vipo 35 tu Rais Dk .Samia anapanga utaratibu wa kutenga fedha ili kuendelea kuwekeza zaidi kujenga chuo cha kisasa kama anavyofanya kwenye sekta nyingine,”.
Kihenzile ameatoa wito ndani na nje ya nchi viwanja vya ndege na usafiri wa anga nchini ni salama kuliko mahali popote kwa sasa, hivyo mashirika,wawekezaji, wafanyabiashara waingie kwenye usafiri wa anga ni salama.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA),Hamza Johari amesema lengo ni kufahamu Mamlaka hiyo na majukum wanayofanya ameridhishwa na kazi ambazo wanafanya.
“Naibu Waziri ametoa maelekezo ikiwemo katika suala zima la miradi kuhakikisha kwamba wanafanya miradi hiyo kwa viwango na ubora unatakiwa na inamalizika kwa wakati,” amesema Johari.
Amesema mradi wa kubadilisha mifumo ya sauti ambayo wanaendelea nayo , kuboresha mawasiliano na mradi wa ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga.
Amesema katika miradi hiyo yote mitatu watahakikisha maelekezo yatafanyiwa kazi kuwa miradi inafanyika kwa ubora na kumalizika kwa wakati kwa viwango vya kimataifa.
Ameongeza kuwa umuhimu wa kuhakikisha wanafuatilia maagizo yote yanayotolewa na viongozi hivyo kila linalo wahusu wao watalifuatilia na kusimamia utekelezaji wake.
Aidha amesema kuongeza kwa mashirika ya ndege wanaamini yakiwa mengi na gharama za nauli zinapungua.