Home BUSINESS MRADI WA KUIMARISHA UZALISHAJI VIWANDANI KUTEKELEZWA TANZANIA BARA NA VISIWANI

MRADI WA KUIMARISHA UZALISHAJI VIWANDANI KUTEKELEZWA TANZANIA BARA NA VISIWANI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Bw. Ali Khamis Juma ametoa rai kwa wajasiliamali na wanafunzi kutumia ipasavyo fursa ya mafunzo ya kuzalisha bidhaa zenye ubora na mbinu za kutafuta masoko yanayotolewa na BDS – KAIZEN.

Ameyasema hayo Novemba 14, 2023 alipokuwa akifungua Mkutano wa Pamoja wa Kamati Tendaji ya utekekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Viwanda vya Uzalishaji kupitia Programu za Huduma za Maendeleo ya Biashara (BDS) na Uboreshaji wa Ubora na Tija (KAIZEN) uliofanyika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),Dar es Salaam.

Amesema Mradi huo unaotekelezwa Tanzania Bara na Visiwani unalenga kuwajengea uwezo Watanzania hususani wajasiliamali katika kuimarisha uzalishaji viwandani na mbinu za utafutaji wa masoko.

 

Vilevile Amesema Mradi huo pia unalenga kuwajengea uwezo wajasiliamali kuzalisha bidhaa zenye viwango zitakazoweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi pamoja na kukuza biashara na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Tanzania inatekeleza Mradi huu Awamu ya tatu kupitia Programu ya KAIZEN chini ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kuanzia 2023 hadi 2027 ukilenga kutoa huduma za kibiashara kwenye sekta mbalimbali kupitia Taasisi za Serikali, Sekta binafsi, Taasisi za elimu

Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi huu ilikiwa 2013 – 2017 na Awamu ya pili ilikiwa 2017 – 2021 ikilenga kuongeza tija na ubora kwenye viwanda na uzalishaji wa bidhaa kwa gharama ndogo nchini.

Previous articleGGML YAIBUKA KAMPUNI INAYOAMINIKA ZAIDI KATIKA TUZO ZA MLAJI
Next articleORYX GAS YASISITIZA MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here