Home LOCAL CCM YATOA MAAGIZO MATANO GEITA

CCM YATOA MAAGIZO MATANO GEITA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda amesema Chama Cha Mapinduzi kinatoa maagizo matano kwa mkoa wa Geita ambayo  yanatakiwa kutekelezwa 

Makonda ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 11, 2023 wakati aliposimama na kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Bwanga akiendelea na ziara yake Mkoani Geita

Maagizo hayo ni pamoja na kushughulikia Malalamiko ya Wafanyabiashara wa Mkaa Chama Cha Mapinduzi kimemtaka Mkuu wa Mkoa kuwapokea, kuwaskiliza na kuchukua hatua za utatuzi kwa Wafabyabiashara hao kwa yeyote mwenye kibali na alidhulumiwa kwa kupokonywa mikaa yake na hata usafiri wake.

Makonda ameongeza kuwa CCM inatoa siku 4 kwa TARURA hadi kufikia siku ya Jumatano tarehe 15 Mkandarasi awepo Bwanga kwa ajili ya Ujenzi wa Stendi daladala.

Akiendelea kutoa maagizo Makonda ameongeza kuwa CCM inamuelekeza Waziri wa Maji Mhe. Aweso kuweka msukumo zaidi kukamilisha utekekezaji wa mradi wa Maji Bwanga kwani tayari fedha shilingi Bilioni 1.6 zimeshatolewa.

Katibu mwenezi huyo pia amesema CCM maelekezo kwa Wakala wa Umeme Vijijini  REA kuhakikisha inakamilisha uwekaji wa taa za Barabarani katika Kata ya Bwanga.

Pamoja na mambo mengine Makonda ameitaka TARURA kuharakisha mchakato wa Ujenzi wa Barabara katika Kata ya Bwanga Wilayani Chato.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here