Home LOCAL BRELA: BRELA YATOA MSAADA KWA WAGONJWA OCEAN ROAD

BRELA: BRELA YATOA MSAADA KWA WAGONJWA OCEAN ROAD

Afisa Habari Mkuu Kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Christina Njovu (kushoto) akikabidhi mahitaji mbalimbali ya wagojwa kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu kwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi wa hospital ya Ocean Road Bi. Mary Haule (kulia), ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Taasisi ya urejeshaji kwa jamii.

Maafisa Kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), waliovaa fulana wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa uongozi wa Hospitali ya Ocean Road (Kutoka kulia)Afisa Ustawi wa Jamii, Bw.Jastine Chambo, (wa tatu kutoka kulia) Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Bi. Mary Haule, mara baada ya kukabidhi mahitaji mbalimbali ya wagonjwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya BRELA ya kurejesha kwa Jamii. Misaada hiyo imekabidhiwa Leo Novemba 3, 2023 katika Hospitali hiyo.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imetoa mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road, Jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi mahitaji hayo leo Novemba 3, 2023 kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa (BRELA), Afisa Habari Mkuu wa BRELA Bi.Christina Njovu amesema kuwa Taasisi imekuwa ikitekeleza Sera ya Urejeshaji kwa Jamii kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji.

Ameongeza kuwa Wakala imekua ikishirikiana na jamii katika kutekeleza majukumu yake, hivyo itaendelea kutoa mahitaji mbalimbali kwa wenye uhitaji wakiwemo wagonjwa, kwa kutambua kuwa ni wadau muhimu katika urasimishaji wa biashara licha ya kukabiliwa na changamoto za kiafya.

Pia ameziomba Taasisi nyingine za Umma na Binafsi kuwa na utaratibu wa kutoa misaada kwa jamii ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwapatia wananchi huduma bora za Afya.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Ocean Road Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Bi.Mary Haule ameishukuru BRELA kwa misaada hiyo kwani kuna wagonjwa mbalimbali wenye uhitaji kwenye hospitali hiyo, hivyo amezitaka Taasisi nyingine kujitokeza kutoa misaada Ili wale wasio na ndugu wala jamaa wapate mahitaji muhimu.

BRELA imetoa misaada ya sabuni, miswaki, diapers, mafuta ya kupaka mwilini, dawa za meno na vitu vingine mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here