Home LOCAL BCEG WATAKIWA KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA...

BCEG WATAKIWA KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA MICHEZO CHA DODOMA

Na Eleuteri Mangi, WUSM

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amemwagiza mkadarasi Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kukamilisha ujenga mradi wa mradi wa kituo cha michezo na eneo la kupumzikia wananchi jijini Dodoma kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Naibu Waziri Mwinjuma amefanya ziara Oktoba 31, 2023 kukagua ujenzi wa mradi huo unaojengwa na Kampuni ya BCEG ya nchini China katika eneo la Nanenane Nzuguni jijini Dodoma.

“Nimetembelea kukagua mradi huu wa ujenzi wa kituo cha michezo hapa Dodoma, huu ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ametuelekeza Wizara kujenga vituo vya michezo na maeneo ya kupumzika wannchi hapa Dodoma na Dar es Salaam” amesema Naibu Waziri Mwinjuma.

Naibu Waziri Mwinjuma amesema mkandarasi huyo anawajibika kusimamia na kufuata mpango wa manunuzi waliojiwekea pamoja na kuongeza idadi ya wafanyakazi ili kufikia malengo ya Serikali na kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kwa awamu ya kwanza ifikapo Mwezi Machi 2024.

Kwa upande wake Meneja Mradi huo kutoka BCEG Li Liang amesema watasimamia na kufanya kazi kulingana na mkataba huo pamoja na maelekezo ambayo viongozi wanayatoa ili kukamisha kazi hiyo kwa wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here