Home BUSINESS WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2023; WANACHAMA WA PSSSF MWANZA WAFURAHIA HUDUMA

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2023; WANACHAMA WA PSSSF MWANZA WAFURAHIA HUDUMA

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSSSF Bw. Fortunatus Magambo (wa pili kutoka kushoto) akiwasikiliza wateja wa PSSSF waliofika katika ofisi za kanda ya ziwa jijini Mwanza kwa ajili ya kupata huduma. Wa kwanza kushoto ni Bw. Rajabu Kinande, Meneja wa kanda ya ziwa na wa tatu kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano na Elimu kwa wanachama Mkuu, Bw. Abdul Njaidi. 

Na: Mwandishi Wetu, Mwanza

Wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) mkoani Mwanza wameupongeza Mfuko huo kwa kuwa karibu na Wanachama wake na kuendelea kutoa huduma bora.

Pongezi hizo zimetolewa na Wanachama hao jijini Mwanza Oktoba 5,2023 wakati wa shamrashamra za wiki ya huduma kwa wateja ambayo inaadhimishwa wiki hii ulimwenguni kote.

Katika kuhakikisha PSSSF inapata mrejesho sahihi kutoka kwa
wanachama wake, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw. Fotunatus Magambo aliongoza timu ya maafisa wa PSSSF kuwatembelea wanachama katika ofisi zao na wastaafu katika makazi yao.

Wakiwa katika ofisi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira
Jijini Mwanza (MWAUWASA), walikutana na Watumishi watatu ambao wote walisema
wanafurahishwa na huduma za PSSSF.

“Kwa kweli mimi wakati nimejifungua sikupata shida kupata fao la uzazi, nililipata kwa wakati, hata hivyo nawashauri akina Mama wengine kuhakikisha wanawasilisha nyaraka zote muhimu ndani ya miezi mitatu baada ya kujifungua ili waweze kupata fao hilo” alifafanua Bi. Monika Emmanueli, Mtumishi wa MWAUWASA.

Naye Bi. Vumilia Jonas, Mtumishi MWAUWASA alishauri, “Ni vyema PSSSF iweke mfumo wa kutoa mrejesho wa Wanachama ili aweze kujua nini kinaendelea katika huduma anayofatilia”.

PSSSF ina huduma mbalimbali za kumwezesha mwanachama kufuatilia huduma jambo lolote juu ya uanachama wake, moja ya huduma hiyo ni PSSSF kiganjani ambapo wanachama anaweza kuhudumiwa kupitia simu janja bila ya kuhitaji kufika kwenye Ofisi za Mfuko.

Pia Bw. Magambo na timu yake walimtembelea daktari Msataafu wa hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Dkt. Gervas Manzi ambaye anaishi Nyamagana jijini Mwanza kwa lengo la kumjua hali na kupata mrejesho wa huduma za PSSSF kwa wastaafu.

“Kwa kweli huduma za Mfuko zipo vizuri, kwa upande wangu nipo
vizuri sana na pensheni yangu naipokea kwa wakati, hata hivyo nashauri PSSSF iendelee kutoa elimu kwa wanachama ili waweze kujua haki zao kabla na baada ya
kustaafu” alishauri Dkt. Manzi.

Wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya
Oktoba, lengo lake ni kuzikumbusha taasisi mbalimbali kutoa huduma bora na za
wakati kwa wateja.

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSSSF Bw. Fortunatus Magambo (kushoto) akisalimiana na wateja wa PSSSF waliofika katika ofisi za kanda ya ziwa jijini Mwanza kwa ajili ya kupata huduma. Wapili kushoto ni Afisa Uhusiano na Elimu kwa wanachama Mkuu, Bw. Abdul Njaidi.
Daktari Msataafu wa hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Dkt. Gervas Manzi, akizungumza na Watumishi wa PSSSF waliomtembelea nyumbani kwake jijini Mwanza. Watumishi wa PSSSF,waliongozwa na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSSSF Bw. Fortunatus Magambo (kushoto) na Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kulia) 

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSSSF Bw. Fortunatus Magambo (katikati) akizungumza na watumishi wa Mfuko huo ofisi za Kanda ya ziwa jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza, Bi. Mariam Mshana (katikati) alipokea mfuko wenye makabrasha ya elimu juu ya PSSSF kutoka kwa Watumishi wa PSSSF wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSSSF Bw. Fortunatus Magambo (wa pili kutoka kushoto)
Bw. Magambo akiagana na mteja baada ya kumuhudumia
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa PSSSF Mwanza baada ya kikao nao kwa lengo la kuwahamasisha kuendelea kutoa huduma bora kwa wanachama. Kushoto waliokaa ni Meneja wa kanda ya ziwa, Bw. Rajabu Kinande.
Previous articleRAIS SAMIA AMWAGA MABILIONI YA FEDHA KILIMANJARO KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO; MBUNGE MALEKO AFUNGUKA
Next articleCOMRED CHONGOLO AKUTANA NA CHIFU WA KABILA LA WAKONONGO KATAVI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here