Home Uncategorized WAZIRI MKUU MAJALIWA KUWA MGENI RASMI MKUTANO MKUU SEKTA YA ANGA NCHINI

WAZIRI MKUU MAJALIWA KUWA MGENI RASMI MKUTANO MKUU SEKTA YA ANGA NCHINI

Na: Mwandishi wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho anatarajia kuwa Mgeni rasmi kwenye mkutano mkubwa wa wadau wa Anga ambao watajadili mambo mbalimbali.

Hayo ameyasema leo Oktoba 29 jijini Dar es na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari wakati wakisheherekea miaka 20 ya TCAA amesema waliamua kuandaa mbio za TCAA Fun Run 2023 katika mbio hizo waliandaa watakao kimbia kilomita 5 na kilomita 10.

Amesema Mamlaka hiyo ilianzishwa mwaka 2003 kufikia mwaka huu imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake hivyo wanaangalia miaka 20 waliotoka na 20 wanayoenda.

“Kesho tunatarajia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kufungua mkutano wa wadau wa Anga na kusherekea miaka 20 ya TCAA na wadau wa anga kwa kujitathimini mafanikio tuliofanya na changamoto zinazowakabili, “amesema Johari.

Amesema jukumu lao ni kuhakikisha wadau wa anga wanafanya shughuli kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa.

Amesema watu walikuwa wanakimbia vizuri na walijiaanda na mbio hizo katika kuweka mwili vizuri na afya njema.

Ametoa wito kwa watanzania wote kujali sana afya zao kwa kula vizuri na kufanya mazoezi kwa sababu ni tiba na yawe sehemu ya maisha yetu.

“Tukiendelea kufanya mazoe mara kwa mara tutaepukana na magonjwa nyemelezi ambayo yanaweza kuhatarisha afya zetu,” amesema .

Aidha amewashukuru wana TCAA , wanangan na wadau wengine ambao wamewaunga mkono katika mbio hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Hashim Komba amesema kuwa miaka 20 ya TCAA ni mageuzi ya Sekta ya anga.

“Leo tulikuwa tunasherekea miaka 20 ya TCAA kwa kumbia mbio za TCAA Fun Run 2023 kufanya mazoezi ni kuhimarisha afya ya akili zetu, “amesema Komba.

Amesema TCAA inatoa huduma kwenye viwanja vya ndege 15 nchi nzima na amempongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha viwanja vya ndege na ununuzi wa ndege.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here