Home BUSINESS TASAC YAFANIKIWA KUKAGUA MELI ZA KIMATAIFA ZAIDI YA 200

TASAC YAFANIKIWA KUKAGUA MELI ZA KIMATAIFA ZAIDI YA 200

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Nelson Mlali, akitoa taarifa kuhusu majukumu na mafanikio ya Shirika hilo ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kukutana na Wahariri na Waandishi wa habari,  kilichofanyika leo Octoba 5,2023 Jijini Dar es Salaam. (Wa pili kulia), ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, na (katikati), ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Erick Mkuti.

  Afisa Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akizungumza wakati wa mkutano huo.

 Mhandisi Said Kaheneko akijibu baadhi ya maswali ya Wahariri katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, akizungumza kwa niaba ya Wahariri waliohudhuria kwenye kikao hicho, kilichofanyika leo Octoba 5,2023 Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa TASAC Bi. Mariam akitoa neno la shukrani kwa wahariri waliohuduria katika kikao kazi hicho, mara baada mapema kabla ya kuhitimishwa kwa kikao kazi hicho.
DAR ES SALAAM

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limefanikiwa kuongeza idadi ya kadhia zilizohudumiwa kutoka kadhia 6,000 mwaka 2019/2020 hadi kufikia z kadhia 10,000 mwaka jana.

TASAC pia imeunda nyenzo za udhibiti wa usafiri majini ikiwa ni pamoja na Kanuni na Miongozo ili kuwezesha utekelezaji wa sheria katika kudhibiti usafiri majini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Nelson Mlali wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari katika mkutano ulioratibiwa na Msajili wa Hazina uliofanyika leo Octoba 5, 2023, Jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, TASAC imeelezea mafanikio iliyoyapata hasa kutokana na usikivu wa Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupokea ushauri wa kitaalam na kutoa maelekezo sahihi kupitia Wizara ya Uchukuzi, na kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali pamoja na kamati za Bunge.

Aidha, wamefanikiwa kuongeza idadi ya watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC, kwa maana ya idadi ya leseni na vyeti vya usajili vilivyotolewa,pamoja na  kuongezeka kwa idadi ya vyeti kwa mabaharia waliokidhi masharti.

Pia, Mlali amesema wamefanikiwa kuimarisha udhibiti wa huduma za bandari baada ya urasimishaji wa maeneo 20 ya kibandari katika mwambao wa bahari na maziwa.

Mlali amesema wamefanikiwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa mikataba, itifaki na miongozo inayotolewa na Shirika la Bahari Duniani (IMO) nakuridhiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbali na hayo, amesema kupata tuzo ya mshindi wa kwanza kitaifa na Kupata cheti cha ubora cha mfumo wa usimamizi wa ubora.

Katika hatua nyingine, Mlali amesema kuwa Shirika hilo linaendelea na utekelezaji wa ujezi wa boti tano za uokozi ambapo mbili zitakuwa ziwa Victoria, mbili Ziwa Tanganyika na moja Ziwa Nyasa.

“Tunatekeleza ujenzi wa boti tano za uokozi ambapo tunataka tuweke pale ziwa Victoria boti mbili, ziwa Tanganyika mbili na pale ziwa Nyasa boti moja, taratibu zimeshaanza kuangalia uwezekano wa kufanya vitu hivyo ili baadae tufike mahala tuweze kuwa na boti hizo za uokozi ambazo zitakuwa tayali kukimbia katika maeneo ya matukio kwenye maeneo ya karibu.

“Kutekeleza mradi wa kimataifa wa mawasiliano na uchukuzi katika ziwa Victoria, ambao ni mpana sana, lengo lake ni kuboresha mawasiliano na kusaidia katika shughuli za uokoaji zinapotokea ajali ili watu waweze kuwasiliana, na msaada wa karibu uweze kufika.

“Ziwa letu ni kubwa katika eneo tunalolimiliki, mradi huu umelenga kuwasaida watu wa kawaida kabisa, kwa hiyo Serikali imefanya jitihada kubwa ili kuwafikiria watu wa chini.” Amesema Mlali.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

Wahariri wakiwa katika picha ya kumbukumbu.

 

Previous articleCOMRED CHONGOLO AKUTANA NA CHIFU WA KABILA LA WAKONONGO KATAVI
Next articleNCHI ZA AFRIKA ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA ONGEZEKO LA IDADI YA WATU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here