Home SPORTS SIMBA SC YAICHAPA  PRISONS 3-1

SIMBA SC YAICHAPA  PRISONS 3-1

TIMU ya Simba SC imetoka nyumba na kushinda mabao 3-1  dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama dakika ya 34, Nahodha na mshambuliaji John Bocco dakika ya 45 na ushei na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 86 kwa penalti, wakati la Prisons limefungwa na Edwin Barua dakika ya 12.
Simba SC inafikisha pointi 12 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC, ikiizidi Azam FC pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga pointi tatu baada ya wote kucheza mechi nne.
Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kipigo cha leo inabaki na pointi moja baada ya kucheza mechi nne ikiendelea kushika mkia.
Mchezo mwingine Singida Big Stars imepata ushindi wa kwanza Ligi kuu baada ya kuichapa bao 1-0 Timu ya Mtibwa Sugar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here