Na: Mwandishi Wetu
Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamepongeza huduma zinazotelewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Kanda ya Mashariki kwa kuwafikia majumbani wastaafu wenye changamoto mbalimbali ikiwemo wale wanaokabiliwa na changamoto za kiafya.
Wakizungumza mara baada ya kufikiwa na Watumishi wa Mfuko,
Oktoba 4, 2023 katika kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja baadhi ya wastaafu wanaoshi pembezoni mwa Manispaa ya Morogoro katika Kata ya Bigwa wamefurahishwa na jitihada za Mfuko katika kupanua zake za uhakiki wa taarifa kwa wagonjwa waliokumbwa na changamoto mbalimbali.
Niwael Mbaga ni miongoni mwa Waastafu anayeishi katika Kata
Bigwa Manispaa ya Morogoro (63) alisema alianza kupata huduma hiyo mara baada ya kustaafu kwake na kuanza kufatilia mafao akiwa katika hali ya ugonjwa uliopelekea kushindwa kufatilia mafao yake ambapo alianza kupata huduma hiyo
akiwa nyumbani kwake.
Aidha mama huyo amewatoa hofu Watumishi wa Umma juu huduma zinaztolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambao unakidhi viwango vya huduma za kimataifa kwa kuwafikia wastaafu pindi wanapokuwa na changamoto za maradhi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bi Grace Kabyemera, amesema Mfuko huo umejidhatiti katika kuwafikiwa wateja woteili waweze kupata huduma kwa urahisi zaidi ambapo wameanza kuandaa mfumommaalumu utakaowawezesha wateja kupata huduma kwa kutumia simu janja.
“Sisi tunamjali kila mteja wetu katika kila hali, kuna wateja
ambao hawawezi kufika ofisini kutokana na changamoto mbalimbali hasa za kiafya hivyo mfumo huu utawawezesha wastaafu kupata huduma zetu kwa wepesi naufanisi zaidi” Alisema Bi Kabyemera.
Naye Meneja wa PSSSF Kanda ya Mashariki, Bi Zaida Mahava,
aliwaasa wastaafu na wanachama wa PSSSF wanaokaribia kustaafu kujihadhari na wimbi la matapeli ambao wanatumia mwanya wa teknolojia kuwalaghai wastaafu kwa kuwaibia.
“Kumekua na wimbi kubwa sana la matapeli, hivyo niwatake wastaafu na wale watumishi wanaokaribia kustaafu kutambua huduma zetu zinatolewa bure, watumie fursa ya ofisi za PSSSF zilizo mikoa yote ya Tanzania na Zanzibar kwa kupata huduma bila gharama yeyote”
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yanaadhimishwa kote duniani wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kwa lengo la kutambua na kuenzi wateja na watoa huduma katika nyanja mbalimbali za kisekta.