Home LOCAL MTENDAJI MKUU TARURA AWATAKA WATUMISHI BUHIGWE KUENDELEA KUFANYA KAZI KWA BIDII

MTENDAJI MKUU TARURA AWATAKA WATUMISHI BUHIGWE KUENDELEA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Buhigwe,Kigoma

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff amekutana na watumishi wa TARURA Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo amepokea taarifa mbalimbali za kiutendaji na kuwataka kuzingatia uadilifu na kutimiza wajibu.

Mhandisi Seff ameyasema hayo alipokuwa kwenye kikao na watumishi wa TARURA wilayani humo kwa lengo la kupata mrejesho na kuangalia kama kuna changamoto ziweze kupatiwa ufumbuzi na watumishi walipata fursa ya kutoa maoni yao lengo likiwa ni kuboresha utendaji ili kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

“Nimepata nafasi ya kumsikiliza kila mmoja wenu na changamoto zilizo ainishwa zitafanyiwa kazi, wito wangu kwenu ni kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu wake kwa wakati na kwa uadilifu ili tuweze kufikia malengo kwa kutoa huduma bora ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi”, amesema Mhandisi Seff.

Mhandisi Seff anaendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi katika Wilaya ya Buhigwe ambapo pia atakagua ujenzi wa Barabara ya Kasulu-Kabanga-Kasumo-Muyama- yenye urefu wa km 36 kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wa km 12.5 unaendelea kwa awamu ya kwanza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here