Home BUSINESS MKURUGENZI MTENDAJI WA AKIBA COMMERCIAL BANK PLC AZINDUA RASMI WIKI YA HUDUMA...

MKURUGENZI MTENDAJI WA AKIBA COMMERCIAL BANK PLC AZINDUA RASMI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba Bw: Silvest Arumasi, amezindua rasmi wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Kijitonyama. Katika uzinduzi huo, Mkurugenzi amewashukuru wateja kwa kuichagua na kuiamini Benki ya Akiba katika kuwahudumia. Aidha, ameendelea kuwaahidi na kuwahakikishia wateja huduma bora kutoka ACB.

Sherehe za huduma kwa wateja zina adhimishwa katika matawi yote ya ACB na hivyo Bw: Arumasi amewaalika wateja wote kutembelea matawi ya Akiba kwa ajili ya kusherekea wiki hii ya huduma kwa wateja pamoja na kupata taarifa mbali mbali za huduma mpya na maboresho mbali mbali. Mwisho kabisa

Mkurugenzi amewashukuru wateja wote walioshiriki katika zoezi la utafiti wa viwango vya uridhikaji katika utoa huduma yaani (Customer Satisfaction Survey) lililoratibiwa na kampuni huru ya kujitegemea kwa lengo la kuhakikisha uwazi na uhuru wa kutoa maoni kwa wateja.

ACB inao utamaduni wa kufanya utafiti huo kila mwaka na hivyo amewasihi wateja kushiriki tena kikamilifu kwa lengo la kupata maoni na mirejesho itakayosaidioa kuboresha huduma zitolewazo.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU OCTOBA 2,2023
Next articleWAKUTANA KUJADILI ITIFAKI ZINAZOSIMAMIWA NA SHIRIKA LA MILIKI UBUNIFU AFRIKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here