Home SPORTS IHEFU SC YAICHAPA BAO 2-1 YANGA SC

IHEFU SC YAICHAPA BAO 2-1 YANGA SC

TIMU ya Ihefu SC imendeleza umwamba kwa mabingwa  Yanga SC baada ya kuituwaza mabao 2-1  mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa  Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.

Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa  kiungo w Pacome Zouazoua dakika ya nne, kabla ya Ihefu kusawazisha kupitia kwa   Lenny Kissu dakika ya 40.

Kipindi cha pili wenyeji walipata bao la pili likifungwa na Charles Ilamfya dakika ya 67.

Kwa ushindi huo, Ihefu inafikisha pointi saba na Yanga inabaki na pointi zake tisa baada ya wote kucheza mechi nne.

Mchezo mwingine timu ya Kagera Sugar imeshindwa kutamba katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba baada ya kulazimishwa sarae ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here