Home LOCAL Dkt. SAMIA: TANZANIA NA UJERUMANI KUDUMISHA USHIRIKIANO

Dkt. SAMIA: TANZANIA NA UJERUMANI KUDUMISHA USHIRIKIANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier wakati wa Mkutano wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujerumani uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu ziara yake nchini Tanzania. Mkutano huo umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ipo tayari kwa mazungumzo yajayo ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani yatakayofanyika mwaka 2024.

Wakizungumza Leo Oktoba 31 na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam Dk. Samia na Rais wa Shirikisho ya Jamhuri ya Ujerumani, Frank Walter Steinmeier wamezungumza kwa pamoja na mambo mengine.

Amesema Lengo la ziara ya Rais wa Ujerumani ni kuhimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Ujerumani uliodumu zaidi ya miaka 60.

Katika hilo wameelekeza timu za wataalamu wa Tanzania na Ujerumani kuendelea na mazungumzo ya mara kwa mara kuboresha maeneo ya ushirikiano na serikali ya Tanzania ipo tayari mazungumzo yajayo ya ushirikiano yatafanyika mwakani,” amesema Dk.Samia.

Amesema nchi imepiga hatua nyingine ya kihistoria katikati uhusiano wake na Ujerumani hapa nchini anamshukuru Rais huyo kwa kubali ziara ya kutembelea Tanzania ni heshima kwake.

Ameeleza kuwa ushirikiano mkubwa baina ya Tanzania na Ujerumani kwenye sekta ya maji, afya, matumizi endelevu ya rasilimali na ulinzi wa mazingira, utawala bora wa fedha, usawa wa kijinsia na michezo.

“Suala la bima ya afya tulitaka usaidizi kwao watusaidie serikali ya Ujerumani inajenga hospitali kubwa ya jeshi Dodoma pia tuliomba watusaidie kujenga hospitali kubwa ya kisasa ya maradhi ya kuambukiza Lugalo,”amesema.

Amesema wanatusaidia kwenye elimu, maji na upande wa scholarship elimu ya ufundi katika mazungumzo yao wamesisitiza umuhimu kukuza ushirikiano huo.

Aidha amesema katika utawala mambo mengi yamepita hivyo kufungua majadiliano na kuona jinsi watakavyoweza kukubaliana kwa yale yaliyopita wakati wa utawala wa Ujerumani hapa nchini vipi wafanya.

“Kufungua majadiliano ya kihistoria vipi watafanya najua kuna familia ambazo zinasubiri mabaki ya ndugu zao yapo Ukatika makumbusho mbalimbali Ujerumani tunafanya mazungumzo tuende nayo vizuri,” amesema.

RAIS WA UJERUMANI

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho Jamhuri ya Ujerumani, Frank Walter Steinmeier amesema kupitia ziara zangu nchini Tanzania nilijifunza kuna makampuni mengi machanga kwaajili ya uwekezaji anatarajia kukutana na wabunifu hao ambao ni vijana wa Kitanzania.

Amesema anatarajia kuonana na vijana wajasiriamali wa Kitanzania wanajihusisha na uvumbuzi wa teknolojia mpy.hususani matumizi ya akili bandia na kuahidi kuwa Ujerumani kusimamia vijana hao kwa kuwapa mitaji na uzoefu kutengeneza ajira kizazi kijacho.

“Nimefurahishwa na hili Ningependa kusema kuwa tutasimama na hawa vijana na ubunifu katika hili swala la ushiriki wa.kiuchumi tukiangalia namna ya kutoa mitaji kwa kuwasaidia kwenye kuongeza uzoefu na maarifa kwenye sekta ya uchumi wa kidigitali,”amesema Dk.Steinmeier.

Amesema wataendelea kusimamia na kutumia fursa zaidi kati ya nchi hizi mbili na kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na wanaweza kusadiana kufanya utafiti wa ndani kuongeza maarifa na akuangalia yaliyopita.

Amesema kupitia kongamano la Jumuiya ya wafanyabishara kati ya Tanzania na Ujerumani kutasaidia kufanya kazi kwa ukaribu na kukuza uchumi na uhusiano kati nchi hizo mbili kuwa na nguvu zaidi hadi kwenye siasa na maeneo mengi zina ushirikiano wa karibu .

Aidha amesema anatarajia kwenda mkoani Ruvuma kuonana na waathirika wa vita vya maji maji.”

Natarajia kuonana na waathirika wa vita vya maji maji na kuzungumza nao na kuangalia kurudisha mabaki yaliyop Ujerumani, “amesema.

Rais wa Shirikisho ya Jamhuri ya Ujerumani yupo nchini kwa ziara ya siku tatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here