Home ENTERTAINMENTS BEN POL KUJA NA ALBUM MPYA YA FLAMINGO HIVI KARIBUNI

BEN POL KUJA NA ALBUM MPYA YA FLAMINGO HIVI KARIBUNI

Na: Neema Adriano

Msanii wa muziki wa Bongofleva na miondoko ya Rnb Bernard Paul ‘Ben Pol’ anatarajia kuzindua Albam yake ya tatu ambayo ameipa jina la Flamingo.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Agosti 6,2023 jijini Dar-es-Salaam amesema kuwa amefanya Album yake ya tatu inayo kwenda kwa jina la Flamingo ambapo album hii inategemewa kuzinduliwa Oktoba 27,2023, katika Hoteli ya Morena, jijini Dodoma.

“Album hii imejawa na vibe kubwa na lakipekee ambapo album hii imesimamiwa na msanii Darasa CMG (Kama Executive Producer) hivyo kutakuwa na nyimbo nane ambazo ni za moto natajia zitapokelewa kwa ukubwa na mashabiki wote wa muziki wangu.

“Uzinduzi huu utaambatana na tour ambayo tutazunguka mikoa kumi na tano na kutakuwa na ngoma za asili kutoka Dodoma.

“Na pia nakwenda kuifanyia Dodoma kwa sababu ni mji ambao nimezaliwa na nimejifunza mengi mazuri hivyo basi nimeona ni vyema nirudishe nyumbani kile kikubwa ambacho ninakifanya kwenye muziki na pia wasanii wengine mbalimbali watakuwepo na listi Yao nitaitangaza hivi karibuni” amesema Benpol.

Nae msanii Shariff Thabit Ramadhani aka Darasa amesema anaheshimu kipaji cha Ben, unajua uwezo mkubwa Ben alionao kuimba na kuperform, na kuwa ni wasanii wachache sana Afrika Mashariki wenye uwezo na kipaji kama cha Ben Pol.

Ikumbukwe Ben Pol ni miongoni mwa wasanii wakongwe waliodumu kwenye chati kwa Zaidi ya miaka 10 licha ya kubadilika kwa zama, na changamoto tofauti tofauti. Hii ni sababu kubwa iliyomfanya aichague jina la albamu yake kuwa “Flamingo”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here