Home BUSINESS AFISA MTENDAJI MKUU BRELA ATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA VIJANA MANYARA

AFISA MTENDAJI MKUU BRELA ATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA VIJANA MANYARA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ametembelea Maonesho ya Wiki ya Vijana leo Oktoba 13, 2023 na kuhamasisha wajasiriamali wanaoshiriki katika maonesho hayo kurasimisha biashara zao.

Bw. Nyaisa amewasihi kutumia fursa iliyopo kwa kufika katika banda la BRELA ili kupata huduma mbambali za sajili na kupata usaidizi kwa wale waliopata changamoto wakati wa kusajili kwenye Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS).

Maonesho hayo yaliyoanza Oktoba 8, 2023 yatahitimishwa kesho Oktoba 14, 2023, sambamba na kilele cha mbio za Mwenge mkoani humo na Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

BRELA inatoa huduma za papo kwa papo za Usajili wa Majina ya Biashara, Usajili wa Kampuni, Usajili wa Alama za Biashara na Huduma, Utoaji wa Leseni za Biashara kundi “A” na Utoaji wa Leseni za Viwanda.b

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here