Home BUSINESS WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMPUNI YA MADINI KUTOKA KOREA KUSINI

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMPUNI YA MADINI KUTOKA KOREA KUSINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe Maalum wa Rais wa Korea Kusini, Bwana Yoon Sang Jick, wakati alipokutana na ujumbe kutoka Korea Kusini uliyoambatana na Makampuni makubwa ya madini, kwenye Ukumbi wa BOT jijijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mjumbe Maalum wa Rais wa Korea Kusini, Bwana Yoon Sang Jick, wakati alipokutana na ujumbe kutoka Korea Kusini uliyoambatana na Makampuni makubwa ya madini, kwenye Ukumbi wa BOT jijijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na ujumbe kutoka Korea Kusini uliyoambatana na Makampuni makubwa ya madini, kwenye Ukumbi wa BOT jijijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Korea Kusini uliyoambatana na Makampuni makubwa ya madini, nje ya Ukumbi wa BOT jijijini Dar es salaam, Septemba 2, 2023(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim amekutana na ujumbe kutoka Korea Kusini uliojumuisha viongozi wa makampuni makubwa ya madini yanayohusika na mnyororo wa thamani wa uzalishaji betri za magari ya Posco Holdings, Posco International,SK, Korea Zinc  na LX International.

Mheshimiwa Majaliwa amewahakikishia wawekezaji hao kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji wao na itawawezesha kuwekeza mitaji yao. “Sisi tuna madini na ninyi ndugu zetu Wakorea mna mitaji, twende tuunganishe nguvu kwa manufaa ya nchi zote.”alisema.

Ameyasema hayo jana (Jumamosi, Septemba 2, 2023) alipokutana na ujumbe wa Korea Kusini na kujadili kuhusu uhushirikiano katika uendelezaji wa madini ya kimkakati nchini Tanzania.

“Ninapenda kuwahakikishia kuwa nchi yetu ni salama na Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya kila linalowezekana kuboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji nchini.”

Waziri Mkuu amesema Serikali imeimarisha mazingira ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya usafirishaji kama barabara, ndege na nishati ya kutosha kwa ajili ya uendeshaji wa viwanda. “Lengo ni kuhakikisha kila muwekezaji anayekuja anapata faida kutokana na uwekezaji wake.”

Kwa upande wake, Mjumbe Maalumu wa Rais wa Korea ambaye ndiye kiongozi wa ujumbe huo kutoka Korea Kusini, Bw. Yoon Sang Jick ameishukuru Serikali ya Tanzania na kwamba wataendelea kushirikiana nayo kuhakikisha malengo ya uwekezaji yanafanikiwa.

Naye, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameishukuru Korea Kusini kwa kuichagua Tanzania nna kufanya mazungumzo kuhusu uwekezaji katika sekta ya madini. Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini humo waje wawekeze Tanzania.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAMOSI, SEPTEMBA 2, 2023.

Previous articleWAZIRI MKUU AMKARIBISHA DKT. BITEKO OFISINI
Next articleRAIS SAMIA AITAKA PAPU KUTUMIA MASHIRIKA YA NDEGE YA AFRIKA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here