Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Noves Mosses (kushoto), alipotembelea Banda la Benki hiyo, kwenye Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya EPZ Bomba mbili leo Septemba 25,2023 Mkoani Geita.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo (kulia), akizungumza alipokuwa katika Banda la BoT wakati wa ziara yake ya kutembelea mabanda, kwenye maonesho ya Teknolojia ya Madini leo Septemba 25,2023, Geita.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kumaliza kutembelea na kuzungumza na Watendaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika maonesho hayo, leo Septemba 25,2023 Geita.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo (katikati), akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Meneja Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Noves Mosses, alipotembelea katika Banda la Benki hiyo kwenye maonesho ya Madini. Geita.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo (wa pili kulia), akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Grace Kingalame (katikati), katika picha ya pamoja na watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)
GEITA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewahimiza wananchi kulinda mazingira kwani yakiharibika uchumi utayumba.
Ametoa kauli hiyo alipotembelea Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita leo Septemba 25, 2023.
Akizungumza wakati akitembelea Banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) alisema bila kutunza mazingira fedha hazitapatikana kwa kuwa shughuli za maendeleo zikiwemo kilimo, uvuvi na mifugo zitayumba.
Dkt. Jafo amesema kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi husababisha ukame ambao huathiri kilimo na mifugo kukosa maji na kufa hali inayosababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo.
“Leo hii kukitokea ukame mifugo itakufa na wakulima watashindwa kulima na yote haya ni mabadiliko ya tabianchi hivyo nawaomba wananchi wapande miti na kutunza mazingra kwa ujumla,” amesema Dkt. Jafo.
Hali kadhalika ametoa rai kwa BoT na kuibenba Sera ya Mazingira kwani ndio ni mojawapo ya injini ya uchumi kwani mazingira yakiharibika na uchumi unadorora.
Ametoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza uchumi kuipitia sekta ya madini na kuimarisha miundombinu.
Aidha, amewapongeza BoT kwa kusimamia vyema fedha pamoja na kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa fedha za kigeni hivi karibuni lakini wameonesha uimara.
Pia, Waziri Dk. Jafo ameitaka taasisi hiyo kusimamia matumizi ya fedha mtandao ili kuwapisha wananchi kutembelea na maburungutu ya fedha hali ambayo si salama.