Home BUSINESS WAKUTANA KUJADILI MFUMO WA LESENI NA TAKWIMU ZA VIWANDA

WAKUTANA KUJADILI MFUMO WA LESENI NA TAKWIMU ZA VIWANDA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imekutana na wawakilishi kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar ili kujadili kwa pamoja jinsi ya utekelezaji wa Sheria ya Taifa ya Utoaji wa Leseni na Usajili wa Viwanda.

Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa akifungua kikao hicho  tarehe 25 Septemba, 2023 katika ofisi za BRELA jijini Dar es Saam amesema kikao hicho ni mwendelezo wa  utekelezaji wa Maelekezo  ya Wizara hizo kutoka pande  mbili za Muungano  ambazo ni Wizara ya Viwanda na Biashara na  Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, maelekezo hayo yanazitaka BRELA na idara ya Maendeleo ya Viwanda Zanzibar kukaa na kujadiliana kuhusu matumizi ya mfumo wa Kielektroniki wa pamoja utakaotumika katika utoaji wa Leseni za Viwanda kwa upande wa Zanzibar na kurahisisha upatikanaji wa Takwimu za Viwanda kwa pande zote mbili za Muungano.

Bw. Nyaisa amesema upande wa Tanzania Bara, Sheria ya Taifa ya Utoaji wa Leseni na Usajili wa Viwanda. imekuwa ikitekelezwa kwa kutoa Leseni za Viwanda na Vyeti vya Usajili ambavyo hutolewa kwa Viwanda Vidogo licha ya Sheria hiyo kuwa na mapungufu mengi kutokana na kutofanyiwa marekebisho kwa muda mrefu.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Viwanda ambaye ndiyo Mkuu wa Msafara kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Dkt. Abdulla R. Abdulla amesema Zanzibar inatarajia kuanza utekelezaji wa Sheria hiyo hivi karibuni, kwa kutumia Mfumo wa utoaji Leseni za Viwanda na Vyeti vya Usajili wa Viwanda vidogo uliyopo BRELA.

Bw. Abulla amesema katika utekelezaji huo Leseni za Viwanda na Vyeti vya Usajili vitakavyotolewa na upande wa Zanzibar havitakuwa na utofauti na vile vinavyotolewa na BRELA kwa upande wa Tanzania Bara.

Hata hivyo amesema kwakuwa  kuna gharama ambazo waombaji wa Leseni za Viwanda na Vyeti vya Usajili ambazo watapaswa kulipia, pande hizi mbili zitaangalia ni  mfumo upi wa malipo utumike ili kufanikisha  utekelezaji wa jambo hilo

BRELA na idara ya Maendeleo ya Viwanda Zanzibar kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar wamekuwa wakikutana mara kwa mara kujadili kuhusu vipengele vilivyopitwa na Wakati katika Sheria ya Taifa ya Utoaji wa Leseni na Usajili wa Viwanda ambayo ilitungwa mwaka 1967.

Pamoja na mambo mengine Sheria hiyo imeipa mamlaka Bodi ya Leseni za Viwanda kutoa Leseni za Viwanda jambo ambalo limepitwa na wakati kutokana na utaratibu unaotumika sasa wa kutumia mifumo ambayo inarahisisha uombaji na utoaji wa Leseni za Viwanda na Vyeti yva Usajili wa Viwanda Vidogo.

Hivyo wataalam wamependekeza Msajili ndiye apewe dhamana ya kutoa Leseni za Viwanda kama ilivyo kwa utoaji wa Vyeti vya Usajili wa Viwanda vidogo na badala yake Bodi ya Leseni za Viwanda ipatiwe ripoti kuhusu Leseni za Viwanda zilitotolewa.

Previous articleWMA YAKAGUA MIZANI INAYOTUMIKA KATIKA SEKTA YA MADINI
Next articleTUMIENI TAALUMA ZENU KITATUA CHANGAMOTO ZA MASUALA YA LISHE KWENYE JAMII
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here