Home BUSINESS WAKULIMA ONGEZENI UZALISHAJI WA MAZAO YA MBEGU ZA MAFUTA YA KULA –...

WAKULIMA ONGEZENI UZALISHAJI WA MAZAO YA MBEGU ZA MAFUTA YA KULA – DKT. KIJAJI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akiwa kwenye Kiwanda cha Wilmar Tanzania Limited kinachozalisha mafuta ya kula ya mawese aina ya Korie na Alizeti aina ya Sundrop pamoja na sabuni ya kufulia ya Foma na Takasa alipofanya ziara kujionea shughuli za uzalishaji kiwandani hapo, kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam Septemba 12, 2023.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akiwa katika Kiwanda cha kutengeneza kamba za plastik na ngazi cha Akberalis Hardware & Electric Limited (Dar Ropes) kujionea shughuli za uzalishaji kiwandani hapo, Jeti, Jijini Dar es Salaam, Septemba 12, 2023

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji(Mb.) ametoa wito kwa Watanzania kuongeza uzalishaji wa mazao ya mbegu za mafuta ya kula hususan alizeti kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya viwanda vya uzalishaji wa mafuta ya kula nchini na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa malighafi hiyo kwa uzalishaji wa mafuta ya kula kwa mwaka mzima.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Septemba 12, 2023 alipofanya ziara katika Kiwanda cha mafuta ya kula ya Korie na Sundrop pamoja na sabuni cha Wilmar Tanzania Limited, na Kiwanda cha kutengeneza kamba za plastik na ngazi cha Akberalis Hardware & Electric Limited (Dar Ropes) vilivyopo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto.

Akiwa katika Kiwanda cha mafuta ya kula ya Korie na Sundrop pamoja na sabuni cha Wilmar Tanzania Limited, Dkt. Kijaji amewahakikishia Watanzania kuwa Kiwanda hicho kinaagiza mafuta ghafi na kuyachakata kupata mafuta ya kula na mabaki hutengenezwa sabuni. Bidhaa hizo huuzwa katika soko la ndani na nje hususani katika soko la EAC na SADC.

Akiwa katika Kiwanda cha kutengeneza kamba za plastik na ngazi cha Akberalis Hardware & Electric Limited (Dar Ropes), Dkt. Kijaji amewashauri Watanzania kununua na kutumia bidhaa zinazalishwa nchini ili kuendelea kuzalisha ajira na kukuza pato la Taifa hususani fedha za kigeni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here