Home BUSINESS WAJASIRIAMALI NA WANANCHI WAHAMASIKA, WAJIUNGA NA NSSF

WAJASIRIAMALI NA WANANCHI WAHAMASIKA, WAJIUNGA NA NSSF

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umetoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wajasiriamali na wananchi katika Maonesho ya Awali Nguvu Kazi/Jua Afrika Mashariki, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam ambapo wajasiriamali kutoka Rwanda na Burundi walishiriki.
 
Afisa Mkuu Uhusiano wa NSSF, Janet Ezekiel, amesema NSSF imeshiriki maonesho hayo kwa kishindo kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wajasiriamali na wananchi.
 
Amesema baada ya mabadiliko ya sheria ya mwaka 2018, NSSF ilipewa dhamana ya kuangalia sekta binafsi na sekta isiyo rasmi wakiwemo wajasiriamali na wale wote waliojiajiri wenyewe.
 
“Kulingana na mpango wa Serikali ikaona kwamba hifadhi ya jamii sio kwa wale tu ambao wameajiriwa katika sekta rasmi bali hata wale waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi kwa sababu kuna wakati hata wao nguvu zitaisha hivyo watahitaji kupata hifadhi hivyo wakijiunga na kuchangia NSSF watanufaika kwa kupata pensheni ya uzee,” amesema.
 
Naye, Abdallah Bashiri ambaye ni Afisa Matekelezo wa Sekta isiyo rasmi, akieleza umuhimu wa hifadhi ya jamii, amesema NSSF imeshiriki maonesho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii katika makundi mbalimbali kama vile wajasiriamali, wakulima, wavuvi, wafugaji na wananchi wengine wote.
 
Amesema NSSF inatekeleza majukumu makuu manne, ikiwemo kuandikisha wanachama kutoka sekta rasmi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao mbalimbali kwa mujibu wa sheria.
 
Amesema baada ya wajasiriamali kujiandikisha wanapaswa kujichangia kila mwezi kwa ajili ya kesho yao iliyokuwa njema ambapo baadaye Mfuko utawalipa mafao kwa wale watakaojichangia kwa muda wa miaka 15 watalipwa pensheni kila mwezi hadi kufa kwao.
 
Amesema Mfuko unatoa mafao ya muda mrefu na muda mfupi ambapo mwanachama mwanamke aliyejichangia kwa muda wa miaka mitatu, atakapojifungua atalipwa mafao ya uzazi, pia kwa mwanachama ambaye atafariki pia atanufaika na mafao ya msaada wa mazishi na pia kuna mafao ya matibabu hivyo aliwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.
 
Abdallah amesema mwanachama ambaye atajiunga kupitia mpango wa hiari, atapata kitambulisho na atatengenezewa namba ya kumbukumbu ya malipo ‘Control number’ ambayo ataitumia kulipia michango yake.
 
“Tumeandaa mifumo rafiki na rahisi ambayo itawawezesha wanachama wetu waweze kujiwekea akiba popote walipo,” amesema.
Afisa Mkuu wa Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Janet Ezekiel akitoa neno la utangulizi ambapo alisema lengo la NSSF kushiriki maonesho ya Awali Nguvu Kazi/Jua Kali Afrika Mashariki ni kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wajasiriamali na wananchi kwa ujumla.
Afisa Mwandamizi sekta isiyo rasmi, Abdallah Bashari akitoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wajasiriamali na wananchi kuhusu umuhimu wa kujichangia kwa ajili ya kutengeneza kesho yao iliyonjema wakati wa maonesho ya Awali Nguvu Kazi/Jua Kali Afrika Mashariki
 
Baadhi ya wananchi wakiwa wanajiunga na Mfuko wa Taifa wa Jamii (NSSF), baada ya kupata elimu ya hifadhi ya jamii.
Matukio katika picha
 
 
 
 
Previous articleADD INTERNATINAL YAWAJENGEA UWEZEZO WATU WENYE ULEMAVU
Next articleWIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAENDELEA KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA WMA KUSIMAMIA RASILIMALI ZA WANYAMAPORI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here