Home BUSINESS WAAJIRIWA WAPYA TUME YA MADINI WATAKIWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA RUSHWA

WAAJIRIWA WAPYA TUME YA MADINI WATAKIWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA RUSHWA

 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amewataka waajiriwa wapya wa kada mbalimbali kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kuendelea kujenga taswira chanya katika Tume ya Madini na Sekta ya Madini kwa ujumla.

Mhandisi Samamba ametoa rai hiyo leo Septemba 20, 2023 jijini Dodoma kwenye ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya wanaotarajia kufanya kazi katika Ofisi za Tume ya Madini zilizopo makao makuu na mikoani.

“Mfahamu ya kuwa Sekta ya Madini ina vishawishi vingi sana, hivyo mnatakiwa kuwa makini kwenye utoaji wa huduma kwa wananchi wanaofika kwenye Ofisi za Madini kwa kutoa huduma kwa kiwango cha ubora wa hali ya juu, ubunifu, uadilifu na bila upendeleo na kuvutia wawekezaji kuwekeza kwenye Sekta ya Madini,” amesema Mhandisi Samamba.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Samamba amesema kuwa wananchi wana matarajio makubwa katika Sekta ya Madini, na kuongeza kuwa Tume ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini kuanzia kwenye utafiti, uchimbaji, uchenjuaji, biashara ya madini, kanuni za ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini ( Local Content) na Wajibu wa Kampuni za Madini kwa Jamii (CSR)

Previous articleRAIS DKT. SAMIA AHITIMISHA ZIARA MIKOA WA KUSINI
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 21-2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here