Home BUSINESS SERIKALI YA ZANZIBAR YATANGAZA KUMPA MWEKEZAJI BANDARI YA MALINDI KWA MIAKA MITANO

SERIKALI YA ZANZIBAR YATANGAZA KUMPA MWEKEZAJI BANDARI YA MALINDI KWA MIAKA MITANO

Na: Halfan Abdulkadir, Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza kuwa Bandari ya Malindi Zanzibar imekabidhiwa rasmi kwa Mwekezaji wa Kampuni ya Africa Global Logistics ( AGL) ya nchini Ufaransa.

Imesema lengo la kufanya Hivyo ni kuongeza ufanisi katika utendaji, na kuondoa utamaduni wa kuendesha Bandari hiyo kimazoea.

Akizungumzia hatua hiyo ya Serikali Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Zanzibar Mahaat Mohd Mahfoudh amesema katika Mkataba huo walioingia utapunguza mrundikano wa makontena kukaa bandarini muda mrefu.

Amesema Makubaliano yaliyoingia kati ya Serikali ya Zanzibar na Kampuni hiyo ya AGL ni Kwa muda wa Miaka 5 au chini ya Miaka hiyo, na kusema kuwa Serikali imesisitiza Kwa Mwekezaji huyo atalinda maslahi ya Rasilimali watu (Wafanyakazi ) ikiwemo Mishahara, likizo, na mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

“Tulichokubaliana sisi watachukua hizi Zana tulizokuwa nazo, na kama Kuna sehemu ambako Kuna mapengo ya Zana basi wao watanunua.” Alisema

“Mchakato ulipita katika Kampuni tofauti ambazo zlikua zimeingia katika kinyang’anyiro Cha kuendesha Bandari ya Malindi na katika ule ushindi Kampuni ya Africa Global Logistics iliibuka mshindi wa hili” aliongeza.

Mkurugenzi huyo amesema faida itakayopatika Bandarini hapo itakwenda kwa Kampuni AGL ambapo itaingia kwa Asilimia 70 na Serikali ya Zanzibar ni Asilimia 30. Hii ikiwa na maana ya kwamba Kwa Kila Dola Moja, sent 30 inaingia Zanzibar .

“Bandari itaendelea kuwa ni ya watu wa Zanzibar, kilichofanyika ni Kuboreshaji wa uendeshaji wabandari na Wala haijauzwa”. alisisitiza na kuongeza kwamba”Watu wafahamu Kampuni hiyo wanakuja kuendesha Bandari ya Malindi tu na wanakuja kuendesha upande wa Kontena na Mzigo Kichele, Yani nimekusudia ukuta Namba 1,2 na 3. Lakini upande wa Bandari ya Abiria utaendelea kuendeshwa na Mamlaka ya Bandari Zanzibar “ Alisema Mahfoudh.

Mkataba huo ulifungwa tangu May 18 na Septemba 18 mwaka huu Mwekezaji ataanza kazi rasmi.

Bandari ya Malindi Zanzibar ilijengwa Mwaka 1920 na ni sehemu ya uchumi mkubwa wa Visiwa hivyo ambapo lengo la Serikali ni kubaibadilisha katika utenda kazi ili uendelee kufanya vyema zaidi kwa maslahi ya Taifa.

Previous articleBRELA YAKUTANA NA TAASISI ZA UDHIBITI KUBORESHA MAZINGIRA YA UFANYAJI BIASHARA NCHINI
Next articleDC MWANZIVA  AZINDUA ZAHANATI CHIMBO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here