Home LOCAL RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MTWARA 

RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MTWARA 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka  wasafirishaji wa korosho kwa malori mkoani Mtwara kupata kibali maalum kutoka  kwa Mkuu wa Mkoa huo.  

Rais Samia amesema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.  

Aidha, Rais Samia amesema lengo la kibali hicho ni kuweza kupata takwimu sahihi  za korosho zinazosafirishwa kutoka mkoani humo kwani wapo wafanyabiashara wanaokwepa kusafirisha kwa njia ya bandari.  

Rais Samia ameagiza kutumika kwa eneo maalum bandarini lililotengwa kwa ajili ya  kupitisha korosho na nafaka nyingine kwa kuwa halitumiki ipasavyo kwa kisingizio  cha uchafuzi unaosababishwa na makaa ya mawe.  

Rais Samia amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuwashughulikia  wafanyabiashara wanaochakachua korosho njiani wanaposafirisha kwa malori kwa  minajili ya kupata faida kubwa ambapo huathiri ubora wa korosho kwenye soko la  dunia. 

Kwa upande mwingine, Rais Samia amezitaka Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa  nchini kushughulikia na kuipa kipaumbele migogoro ya wakulima na wafugaji katika  maeneo yao. 

Awali, Rais Samia alikagua miradi ya maendeleo ikiwemo uzinduzi wa Hospitali ya  Rufaa ya Kanda ya Kusini, chujio la maji la Mangamba, ukarabati wa kiwanja cha  ndege, barabara ya Mtwara–Mnivata (km 50) na kukagua shughuli za uimarishwaji wa bandari.  

Zuhura Yunus 

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Previous articleRAIS DKT. SAMIA AZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA KIMKAKATI MKOANI MTWARA
Next articleTAASISI ZA UDHIBITI ZAELEZWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI YA UFANYAJI BIASHARA NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here